HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 17, 2019

Tigo yazindua duka Kigoma

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza na wakazi wa Kigoma pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo Mkoani Kigoma, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akihakiki utendaji kazi wa mfumo wa kusajili namba za simu kwa alama za vidole katika duka jipya la Tigo lililopo eneo la Lubengela Mkoani Kigoma jana mara baada ya kuzindua duka hilo.Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati.


Na Mwandishi Wetu, Kigoma
 
 KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania imezindua duka jipya mkoani Kigoma hali ambayo itawezesha
watejawa wake kupata huduma zilizoboreshwa zaidi.

Duka hilo jipya litakuwa sehemu maalumu kwa ajili ya wateja kujionea na kufanya majaribio ya bidhaa na huduma mbalimbali mpya na za kidigitali kama TigoPesa zitolewazo na kampuni hiyo.

Wateja pia wataweza kupata huduma ya kusajili upya namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenziwa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati alisema.  “Ufunguzi wa duka hili ni utekelezaji wa mkakati wa Tigo wakufikisha huduma karibu na wateja na tunaamini kuwa duka hili litatoa fursa za biashara kwa wateja na kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani hapa,”.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliipongeza Tigo kwa
jitihada zake za kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye viwango vya kimataifa maeneo yote ya nchi.

“Duka hili jipya litakuwa chachu katika uboreshaji wa huduma za mawasiliano hapa mkoani Kigoma. Mkoa huu una wakazi wachapa kazi na wafanyabiashara ambao wanatamani kujikwamua kiuchumi hivyo hii ni fursa muhimu kwao,” alisema.

Aliongeza  “Hii ni faraja kuona kwamba sasa huduma za Tigo zitapatikana kwa urahisi zaidi na hii itasaidia kufungua fursa nyingi za kiuchumi.”

Duka hilo linapatikana katika mtaa wa Lubenge la Kigoma Mjini, ni la kwanza mkoani humo na litakuwa likitoa huduma sambamba na dawati la wateja lililopo wilayani Kasulu. Duka hili limewekwa katika eneo hili kimkakati ilikufikika kwa urahisi kwa wakazi.

Duka hilo linaifanya Tigo kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma zake maeneo mbalimbali ya nchi ilikufikia wateja wake zaidi ya milioni 11.6 jambo linalofungua milango kwa wateja kufurahia huduma za kidigitali zinazotolewa na kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages