HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 05, 2020

Kampeni ya kuzuia watoto chini ya miaka 18 kutocheza michezo ya kubahatisha yazinduliwa

Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Mohamed (kulia) akiwana mikono huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe.


Na Mwandishi Wetu

BODI ya michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT) imeanzisha kampeni maalum ya miezi mitatu ambayo inalenga kuzuia ushiriki wa watoto walio  chini ya miaka 18 kucheza michezo ya kubahatisha.

Kampeni hiyo iliyoanza Julai na inatarajia kumalizika Septemba mwaka huu, imeanzishwa ikiwa ni baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watu kuwa baadhi ya sehemu zinaendesha michezo hiyo huku watoto walio cjini ya miaka 18 wakishiriki.

Mbali na kampeni hiyo pia bodi hiyo imesema kuwa iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mfumo ambao utasimamia mashine zote za michezo ya kubahatisha ambayo pia itaweka urahisi kuwabaini wanaoendesha shughuli hizo kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja vya maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa,  Mkurugenzi Mkuu wa GBT, James Mbalwe amesema
Mwaka huu watafanya utafiti ili kujua ukubwa wa tatizo hilo la mashine.

"Sasa tumeanza na kampeni ambayo itamfanya hata mtu mzima anapomuona mtoto anashiriki katika michezo hii atoe taarifa polisi au bodi ya michezo ya kubahatisha,” amesema  Mbalwe

Hata hivyo Mbalwe amesema kuwa changamoto kubwa ipo kwa baadhi ya watu wanaoendesha biashara kinyume na utaratibu ambao huweka mashine hizo sehemu yoyote ambayo watoto pia huweza kuzitumia.

“Lakini pindi tu mfumo wetu utakapokamilika itakua ni rahisi kufuatilia mashine zote hata kama zimewekwa kwa siri zitaonekana tu,” amesema

Katika hatua nyingine, Mbalwe amesema licha ya sekta zote kukumbwa na athari za uwepo wa virusi vya corona lakini mapato katika michezo ya kubahatisha yameanza kuongezeka kuanzia wiki ya mwisho ya mwezi Juni.

Katika wiki hiyo ya mwisho mapato yaliyokusanywa yalifikia Sh. Bilioni nane  huku akibainisha kuwa ni matumaini yake kuwa namba zitabadilika

Licha ya kuwa sekta hiyo imeanza kukua tena lakini mapato katika mwaka wa fedha 2020/2021 yatapungua kuliko matarajio yao ya awali ya kukusanya Sh. Bilioni 100.

Katika hatua nyingine ya kulinda watu wanaotembelea maonyesho ya sabasaba dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona bodi hiyo imetoa msaada wa matanki 10 na sabuni za kunawia vilivyo na thamani ya Sh. Milioni15  kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TanTrade).

No comments:

Post a Comment

Pages