Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchmbi (wa nne kutoka kushoto) akiwaongoza wadau
waliofika kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara
ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami kuomba
Dua ili mradi huo ukamilike kwa wakati bila kukwamishwa na changamoto
mbalimbali. Sherehe hizo zilifanyika kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) na ujumbe
alioambatana nao wakikagua magari yanayotumika kwenye ujenzi wa barabara
ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami Mapema
jana wakati wa maadhimisho ya kusherehekea kuanza kwa ujenzi wa mradi
huo yaliyofanyika Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa, wengine pichani ni
wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga
barabara hiyo yenye urefu wa 88.8 KM.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi Dereva Abuu Ally
Funguo ya kuwashia mitambo ya kujengea barabara kuashiria kuanza rasmi
kwa Ujenzi wa Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa
kiwango cha lami wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa
mradi huo zilizofanyika kijijini Kolo
Wilayani Kondoa. Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini Mhe.
Zabein Mhita.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (Katikati mwenye kilemba) na
ujumbe alioambatana nao wakipatiwa maelezo ya mradi wa barabara kutoka
Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kutoka kwa wakandarasi wa Kampuni
inayojenga barabara hiyo ya China Railway Seventh Group.
Wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga
barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kipande cha
Bonga-Mela (88.8KM) kwa kiwango cha lami wakisikiliza salamu ya Mkuu wa
Mkoa Dodoma (Hayupo pichani) wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa
ujenzi wa mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wadau, Mafundi na Wataalamu wa Kampuni ya China
Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi
Bonga Babati kwa kiwango cha lami kipande cha Bonga-Mela (88.8KM).
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa waliojitokeza kwa
wingi kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya
kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Dodoma. Picha na John Banda wa Pamoja Blog.











No comments:
Post a Comment