Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimpokea mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Siku ya Wanawake Dunia lililoandaliwa na Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wa Viongozi, Germina Lukuvi.
Mkurugenzi wa Utafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia) akiongoza msafara wa mgeni rasmi wakati akiwasili katika Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Benki ya CRDB.
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda (wa pili kulia) akipokea hundi
ya shs. milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles
Kimei kwa ajili ya kutambua juhudi
zake za kupambana na mauaji ya albino. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Wanawake wa Viongozi, Germina Lukuvi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam jana, wakati wa kongamano la Siku ya Wanawake Duniani
lililoandaliwa na Benki ya CRDB. Wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtenadji
wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka.
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wa Viongozi, Germina Lukuvi (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia)
Baadhi ya wageni wakijiandikisha.Mama Tunu Pinda akicheza muziki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika Kongamano hilo.
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda akizungumza katika Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Benki ya CRDB.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 10, mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda (wa pili kushoto) kwa ajili ya Chama cha Wake wa Viongozi 'New Millenium Women Group'
Mada zikitolewa
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda akiagana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda akiagana na Mkurugenzi wa Utafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiagana na mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda.
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu
Pinda (wa pili kulia) akiwaongoza kucheza muziki baadhi ya wageni waliohudhulia Kongamano
la Siku ya Wanawake Dunia lililoandaliwa na Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wake wa Viongozi, Germina Lukuvi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na Mkurugenzi wa Utafiti, Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
MKE wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda amesema kuwa
pamoja na juhudi zinazofanywa na taasisi mbalimbali za kumkomboa mwanamke bado
kumekuwa na vitendo vya kikatili na uzalilishaji dhidi ya wanawake.
Mama Pinda aliyasema hayo jijini Dar es
Slaam katika Kongamano la Siku ya Wanawake Dunia lililoandaliwa na benki ya
CRDB.
Alisema bado pia jamii nyingi nchini zinamtazama
mwanamke kama chombo cha starehe huku
zikisahau kuwa ni mtu muhimu katika maendeleo ya Taifa na familia.
“Ni kweli kwamba wanawake wamekuwa wakinyanyaswa
kwa kupigwa na kufanyiwa vitendo vya kikatili, na bado jamii nyingi zinashindwa
kutambua kuwa mwanamke ni mtu muhimu sana katika taifa hili, hivyo ni lazima kukemea
vitendo hivi vinavyofanywa na baadhi ya watu,” alisema.
Alisema wanawake wengi wanashindwa kupiga hatua
kutokana na kutokuwa na fedha hali inayowafanya kuwa tegemezi kwa kila kitu.
“Tunataka kuhakikisha kwamba wanawake wa Tanzania
wanajikomboa katika janga hili la umaskini, ili waweze kujikomboa ni lazima
wapate mikopo kutoka katika benki mbalimbali ili iweze kuwasaidia katika
biashara zao.
“Nataka kuwakomboa wakinamama wengi zaidi
kiuchumi, hivyo basi nawaomba wakinamama wenzangu kukopa mikopo katika benki ya
CRDB na tukipata fedha tusizisahau familia zetu,” alisema.
Mama Tunu alisema hakuna njia rahisi ya mwanamke
kujikomboa kiuchumi hivyo kujituma na kujiamini kwao ndiyo siraha kubwa katika kufikia
malengo waliojiwekea.
“Napenda kuwaambia wanawake wenzangu hakuna njia
ya mkato katika kutafuta mafanikio ni lazima kujituma na kujiamini kuwa unaweza
hata bila ya kuwezeshwa, natoa rai kuwa ukimsaidia mwanamke kupata mkopo
umeisaidia serikali kupata fedha kwani wanawake wote wanapenda kulipa kodi,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles
Kimei alisema kwa kutambua umuhimu wa mwanamke benki yake imeanzisha akaunti
maalum itakayomuwezesha mwanamke kupata mkopo kwa njia rahisi.
Alisema kwa kutambua pia juhudi za mama Tunu
katika kupambana na mauaji wa albino benki yake imetoa kiasi cha Tsh milioni 20
kwaajili ya kusaidia taasisi ya ‘New Millenium women group’ inayoongwa na wake
wa viongozi mbalimbali nchini.
Aidha Dk. Kimei alisema wakinamama wanatakiwa
kuwa na utayali wa kujiwezesha na kupata elimu itakayowasaidia katika
uendeshaji wa biashara zao.
“Ni lazima wakinamama wenyewe wawe na utayali wa
kujiwezesha kwanza wajifunze na kuongeza elimu ya kibiashara kama
kweli wanaghitaji kufanikiwa,” alisema.
No comments:
Post a Comment