Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la Okwi.
Kikosi cha Yanga.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao pekee la ushindi la timu
yao lililofungwa na mshambuliaji, Emmanuel Okwi katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Soka Tanzania bara dhidi ya Yanga uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic (kulia) akisalimiana na kocha
wa Yanga, Hans Van Pluijm kabla ya pambano lao.
Mshambuliaji waSimba, Emmanuel Okwi akimiliki mpira huku
akizongwa na beki wa Yanga, Kelvin Yondani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka
Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha
wa Simba, Goran Kopunovic akishangilia bao lililofungwa na Emmanuel Okwi.
Walemavu wa ngozi albino wakiingia
uwanjani wakati wa mchezo wa Simba na Yanga huku wakiwa wamebeba bango lenye
ujumbe mahsusi uliokuwa ukisomeka ‘Imetosha Mauaji ya Albino’.
No comments:
Post a Comment