Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kukutana na watendaji wa Kampuni
ya Reli Tanzania (TRL). Kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba na
Naibu Katibu Mkuu, Monica Mwamunyange. (Picha na Francis Dande)
WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesitisha uingizaji
wa mabewa 124 yaliyobaki kutoka nchini India hadi atakapopata ripoti ya
uchunguzi wa mabewa ya mizigo 150 yaliyochini utakapokamilika.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Sitta, alisema kama
kuna watendaji wamefikia hatua ya kuingiza mabehewa yaliyochini ya kiwango basi
hiyo ni sawa na hujuma.
Alisema kuwa uchunguzi wa mabehewa hayo 150 ulikuwa
ukifanywa na Kamati Uchunguzi iliyoundwa na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Dk.
Harrison Mwakyembe, unatarajiwa kukamilika siku ya Ijumaa Machi 13 mwaka huu.
“Waziri aliyenitangulia aliteua kamati kupitia Bodi
nisema kuwa uwamuzi huu ni sahii na mimi na unga mkono kwani uamuzi huu unatokana na ukweli kwamba mabehewa haya kuwa
makuu hali inayosabisha mabehewa hayo kuwanguka kwa wastani wa Desemba mwaka
jana yalikuwa yakianguka kila siku yawapo njiani hali inayosababisha hasara kwa
nchi.
“Nimemuagiza Mwenyekiti wa Bodi Bodi ya TRL kukutana
na Kamati ya uchunguzi siku ya Ijumaa ili kupitia taarifa hiyo na
watakapomaliza wahakikishe kuwa hadi
Ijuma 16 iwe imenifikia ofisini kwangu ili kupata taarifa kamili kuhusu
mabewa haya,”alisema Sitta.
Sitta alisema endapo taarifa ya uchunguzi huo
itabainisha kuwa kulikuwa na ubabaishaji katika manunuzi ya mabehewa hayo 150,
Serikali haita sita kuvunja mkataba huo
kwa kutumia sheria ya manunuzi.
Aliema licha ya kuvunja mkataba huo pia kunauwezekano
mkubwa kumshitaki mhusika, kuaangalia kuwa ni nani mwingine amehusika kwenda
kuangalia mabehewa hayo na kufikia hatua ya kupewa mabehewa hayo mabovu.
Alisema ikishindikana kuvunja mkataba huo basi itabidi
wahusika walazimishwe kusimamia gharama za matengenezo ya mabehewa hayo ambayo
tayari yamekwisha ingizwa nchi.
Sitta, alisema pia Serikali itaangalia ni nani alihusika
kwenda kukagua kasha akakubali nchi ipate kitu kibovu, akibainika kutokana,
uzembe huo na kuliletea hasara taifabasi ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheri
Aidha, alisema kuwa hali ya Shirika hili inazidi kuwa
bora siku hadi siku hususani katika upande wa mapato.
Sitta, alisema katika kipindi cha Desemba mwaka jana,
Shirika limeweza kuzalisha kiwango cha dola za kimarekani 140 ukilinganisha na
kiwango cha dola 30 Junuali huo huo, ambacho hicho ndio cha chini kabisa.
“Pia tumepata taarifa kuwa hali ya usafiri wa abiria
unazidi kuimarika kwani hivi sasa kuna vichwa 60 ambapo mahitaji ni vichwa 107
lakini kwa kuwa na hivi hari si mbaya,”alisema Sitta.
Akizungumzia kuhusu watumishi, Sitta, alisema
watumishi wanapaswa kulipwa kama mikataba yao
inavyoonesha katika makubaliano yao.
No comments:
Post a Comment