Geita Gold Mine kwa kushirikia na TACAIDS wameungana kupambana na Virusi vya UKIMWI katika uzinduzi wa upandaji Mlima kwa mwaka huu jijini Dar es SalaamIjumaatarehe 20 Mei.
Kwamujibu wa takwimu kutoka Tumeya Kupamba na UKIMWI nchini (TACAIDS) inakadiriwa kuwa watu milioni 1.6 nchini wanaishi na VVU na Ukimwi. Ugonjwa huu umewaathiri zaidi Vijana na watoto yatima zaidi ya milioni 1.3.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam Makamu wa Rais wa miradi endelevu wa Anglogold Ashanti (GGM) Bw. Simon Shayo amesema Bado ipo changamoto kwa jamii kuhusu elimu ya ugonjwa huo kwa kuwa kuna vituo vichache sana vya taarifa juu ya janga hilo. Amesema
Hali hii ndiyo inayosababisha tuchelewe kukabiliana na janga hili.
Waathirika wa tatizo hili wamekua wawoga kwahofu ya unyanyapaa miongoni mwa jamii. Vile vile alieleza kuwa Usiri na elimu ndogo ya kukabiliana na ugonjwa huu ikiwemo matumizi sahihi ya kinga na dawa zakupunguza makali yake vimezidi kufanya hali ya maambukizi izidi mbaya.
Katika kukabilia na na changamoto hiyo nakuisaidia serikali kufikia lengo namba tatu la Malengo endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa mataifa ya kuwa najamii yenye afya bora ifikapo 2030,Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwakushirikiana na Tume ya Kupambana na UKIMWI nchini (TACAIDS) umendelea tena kuchangisha fedha ili kupambana na UKIMWI kupitia Kampeniyake ya KILI CHALLENGE.
KILI CHALLENGE nikampeni iliyoanza mwaka 2002 ambayo hufanywa kila mwaka kwa wadau mbalimbali kupanda mlima Kilimanjaro na kuchangisha fedha kwa ajiliya kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI pamoja na UKIMWI. Mwaka 2015 pekee Kampeni hii ilifanikiwa kukusanya takribani shilingi za Kitanzania Bilioni Moja.
Fedha hizo zitatolewa kwa wadau mbalimbali wanaojishughulisha na mapambano ya Ukimwi katika uzinduzi wa upandaji Mlima kwa mwaka huu pale Hyatt Hotel, Dar es Salaam Ijumaa 20 Mei,2016 na Mgeni rasmi atakua makamu wa Raisi Mhe. Samia Suluhu. Makamu wa Rais wa miradi endelevu wa Anglogold Ashanti (GGM) Bw. Simon Shayo amesema kuwa Kampeni ya Kili Challenge mwaka huu itakuwa na utofauti mkubwa kwa kuwa inafanyika chini ya Serikali mpya.
“Kwa miaka 15 iliyopita tumeshirikia na vizuri na Serikali ya Tanzania zote, Zaidi ya Asasi 30 zimeweza kunufaika na Mfuko huu katika kipindi cha miaka 15 iliyopita. Baadhi ya asasi hizi ni pamoja na TACAIDS, Benjamin Mkapa Foundation na Geita Hospital. Nyinginezo,”alisema Bw.Shayo.
No comments:
Post a Comment