Chama cha
soka mkoa wa Dar e Salaam DRFA kimempongeza Yusuph Manji kwa kuchaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa klabu
ya Young Africans kufuatia uchaguzi uliofanyika juni 11,2016 katika ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa
DRFA, Almas Kasongo amesema kitendo cha Manji kupata kura nyingi ni ishara tosha
kwamba anakubalika na wanachama wa klabu hiyo licha ya kuwa hakuwa na mpinzani
kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya mwenyekiti.
Kasongo amemuhakikishia
Yusuph Manji kuwa DRFA itaendeleza
ushirikiano uliopo na uongozi wake pamoja na kamati nzima ya utendaji ya Yanga
katika masuala mbalimbali ya kuendeleza soka la Dar es salaam.
Yusuph Manji ameitetea tena nafasi hiyo kwa kupata kura 1,468
kati ya kura zote 1,470 zilizopigwa na kufufua tena matumaini ya wanachama na
mashabiki wa Yanga.
Mbali na
Manji,Kasongo amempongeza pia Clement Sanga kwa kurudi tena kwenye nafasi ya
umakamu mwenyekiti baada ya kutangazwa mshindi kwa kupata kura 1,428.
IMETOLEWA NA CHAMA CHA SOKA MKOA WA
DAR ES SALAAM,DRFA


No comments:
Post a Comment