Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kushoto), muda mfupi baada ya Sherehe ya Kumwapisha
iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba (Kushoto), akikaribishwa Makao Makao ya
Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rwegasira.Katikati ni Naibu
Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu
Mkuu Balozi Yahya Simba.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia
ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara
hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao
Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake.
Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi).


No comments:
Post a Comment