HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2017

RAIS WA CHEMBA YA BIASHARA, VIWANDA NA KILIMO AHIMIZA WATANZANIA KUTUMIA FURSA YA SOKO LA AWALI

Rais  wa Chemba ya Biashara,viwanda na kilimo, Ndibalema Mayanja, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa Mikoa ya Mwanza na Kagera kuchangamkia soko la awali la hisa za TCCIA Investment PLC.


Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa mikoa hiyo bwana Mayanja  alisema “TCCIA Investment PLC ni kampuni ya uwekezaji wa pamoja, imara na inafanya vizuri sana kwani tangu ianzishwe mwaka 2005 ikiwa na mtaji wa shilingi Bilion 1.97 imeweza kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6 na imekuwa ikilipa gawiwo kwa wanahisa wake. Hii ni fursa muhimu na adhimu muitumie kabla ya tar 14 mwezi huu March. “ alisema Mayanga

Rais huyo wa Chemba akiwa ziarani mkoani Mwanza na Kagera pia alifanya kazi ya kujenga uhai wa chemba kwa kukutana na viongozi mbalimbali katika mikoa hiyo.
 Baadhi ya wafanyabiashara na wakzi wa Mkoani  Kagera waliohudhuria kwenye mkutano huo.
 Mshauri TCCIA Mkoani Mwanza, Lazzaro akitoa neno la shukrani kabla ya mkutano kuanza, kulia ni Rais wa TCCIA Ndibalema Mayanja.
 Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA, Ndibalema John Mayanja (katikati), akizungumza hii leo Jijini Mwanza kwenye mkutano na wadau mbalimbali wa biashara. Kulia ni Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leo.
Rais wa TCCIA Ndibalema John Mayanja akizungumza na wafanyabiashara waliohudhuria kwenye mkutano  huo mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment

Pages