Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwakabidhi hati ya usajili wa chama
viongozi wa chama cha ushirika cha Igembe Sabo cha Bunda , Malongo
Mashimo ambaye ni Katibu (kulia) na Maria Nengwa ambaye ni Mwenyekiti wa
Ujenzi baada ya kuzindua ushirika huo akiwa katika ziara ya mkoa wa
Mara, Januari 19, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ameyasema
hayo leo (Ijumaa, Januari 19, 2018) wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua zahanati ya
Hunyari wilayani Bunda, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara.
“Ni
marufuku kwa wanunuzi wa pamba kulima pamoja na wakulima kwa sababu wakulima
wanakosa uamuzi wa kupanga bei. Kuanzia sasa zao hilo litauzwa kwa njia ya
mnada.”
Amesema Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha mazao
makuu ya biashara ambayo uzalishaji wake umeanza kupungua likiwemo na zao la
pamba.
Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kushiriki
kikamilifu katika usimamizi wa kilimo cha zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi
ya shamba, pembejeo hadi masoko.
Pia Waziri Mkuu amewaagiza Maofisa Kilimo katika wilaya
hiyo wawafuate wakulima vijijini kwa ajili ya kutoa elimu itakayowawezesha wakulima kulima kwa kufuata njia bora za
kisasa.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu
amewataka wafugaji kuhakikisha wanakuwa na idadi ya mifugo kulingana na uwezo
wa eneo lao.“Marufuku kulisha mifugo katika mashamba ya watu.”
Amesema Serikali itachukua hatua kali za kisheria
kwa mfugaji yeyote atakayelisha mifugo yake katika mashamba ya wakulima kwani
tabia hiyo huchangia migogo baina yao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JANUARI 19, 2018.
No comments:
Post a Comment