MASHINDANO ya Mbio za Kupokezana Vijiti ‘Relay’ Taifa yaliyokuwa
yafanyike kesho Jumamosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, sasa yamesogezwa
mbele hadi keshokutwa Jumapili.
Sababu
za kusogezwa mbele kwa siku moja mashindano hayo, ni kutoa nafasi kwa wachezaji
kufika jijini Dar es Salaam, baada ya baadhi yao kukabiliwa na changamoto ya
usafiri, ambapo wengi wao watafika Jumamosi.
Mashindano hayo yatashirikisha mbio za mita 100X4 na 400X4
yakishirikisha wanariadha kutoka mikoa tisa waliofikia viwango maalumu
vilivyowekwa na Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).
Mashindano hayo, yanafanyika baada ya mikoa mbalimbali kuendesha
mashindano ‘Trials’ na wale wanariadha waliofikia viwango vilivyowekwa na
Kamati ya Ufundi ya RT, ndio wanakutana katika fainali Jumapili.
“Tunaamini viongozi wa mikoa wamezingatia
viwango tulivyotoa na hakuna udanganyifu, hivyo tunategemea ushindani utakuwa
mkubwa sana na tutapata timu nzuri,”.
Tunawaomba
wadau na wapenzi wa michezo, kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa Jumapili
kushuhudia mbio hizo na kuwapa hamasa wachezaji, kiingilio ni bure.
Wanariadha watakaoshiriki na wanakotoka kwenye mabano ni
Winfrida Makenji, Emmy Hosea, Ali Khamis Gulam, Hassan Khamis Ali, Naima Ali
Musa, Abdallah Issa Khamis , Mohammed Ali Mshamba na Simai Kombo Haji
(Zanzibar).
Wengine ni Binamunzi Katunzi, Ismail Tossil na Diana Matemu
(Dodoma), Daniel Mussa, Elisha Machungwa, Japhet Kitungu (Mara), Boniface
Inalo, Benjamin Michael, Jumanne Chacha, Andrea Robi (Arusha), Elias Sylvester,
Selemani Sabin a Jeremiah Baruti (Dar es Salam).
Pia wamo Ramadhan Omary, Fahadi Juma, Petro Joseph (Singida),
Jacob Lugaila (Mwanza), Bora Hassan (Tabora), Matondo Magembe, Rose Lucas,
Thereza Benard, Rahel Nilla (Simiyu), Benedictor Mathias, Regina Mpigachai,
Pili Mipawa, Amos Charles (Pwani), Elias Sylvester, Selemani Sabi na Jeremiah
Baruti (Dar es Salaam).
IMETOLEWA
NA:
Tullo
Chambo
Msemaji
RT
0752
46 21 03
21 /FEBRUARI/
2020
No comments:
Post a Comment