*Ni kuhusu maelekezo ya utoaji wa vutambulisho vya Taifa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Viongozi na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya (CCM) Mkoa wa Kagera, kwenye ukumbi ELCT Bukoba Hotel, Februari 20, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Kagera Costancia Buhiye, wakati akiwasili katika uwanja wa ndege wa
Bukoka, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti Februari 20, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Viongozi na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya (CCM) Mkoa wa Kagera, kwenye ukumbi ELCT Bukoba Hotel, Februari 20, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeagiza umakini ufanyike katika
utoaji wa vitambulisho vya Taifa hususani katika mikoa ya mipakani si
kwa lengo la kutaka kumkomoa mtu bali ni kwa ajili ya kuimarisha usalama
wa nchi.
Ameyasema
hayo leo (Alhamisi, Februari 20, 2020) baada ya kupokea malalamiko
kutoka kwa wabunge wa mkoa wa Kagera kuhusu usumbufu wanaoupata baadhi
ya wananchi wanapofuatilia vitambulisho vya Taifa kwani wengine
wanadaiwa kuwa si raia.
Malalamiko
hayo yametolewa wakati Waziri Mkuu akizungumza katika Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera. Waziri Mkuu
ni mlezi wa CCM wa mkoa wa Kagera.
“Watu
fuate taratibu katika suala ugawaji wa vitambulisho, Idara ya Uhamiaji
wafuatilie kwa umakini kwa sababu lazima usalama wa nchi usimamiwe
ipasavyo hususani katika mikoa ya mipakani. Watanzania mnatakiwa muwe
makini msiruhusu watu kuingia kwa njia za panya kwani watu hao hawana
nia njema.”
Waziri
Mkuu amesema lazima zoezi hilo lifanyike vizuri na wataharakisha ili
wananchi waweze kupata vitambulisho. Tayari Serikali imeshaongeza vifaa
na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili waweze
kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Wakati huo huo,
Waziri Mkuu amewataka viongozi na wanachama wa CCM waimarishe
mshikamano miongoni mwao na pale kwenye dosari zirekebishwe kwa sababu
hakuna jambo lisiloweza kutatuliwa.
“Tunahitaji
kuwa na umoja na mshikamano ndani ya chama ili sote kwa pamoja tuweze
kufikia malengo tuliyojiwekea….Hata katiba yetu ya chama inatuhimiza
tushikamane kwani wote tunajenga nyumba moja hivyo hatuna sababu ya
kugombea fito.”
Waziri
Mkuu amesema lazima wahakikishe kuwa chama cha CCM kinabaki salama na
kinaendelea kushika dola. “Ni wajibu wa kila kiongozi na mwanachama
kuwezesha malengo hayo kutimia na ni lazima kila tawi litafakari namna
ya kukiwezesha chama kujitegemea kiuchumi.”
Pia,
Waziri Mkuu amewataka viongozi na wanachama wa CCM wajiepushe na suala
la ukabila na udini katika kuteua mtu wa kugombea nafasi mbalimbali
ndani ya chama hicho na badala yake wateue mtu ambaye anauzika ndani na
nje ya chama.
No comments:
Post a Comment