Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akisistiza jambo. (Picha na Maktaba).
Na
Mwandishi Wetu - ORPP
Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ametoa wito kwa vyama vya siasa kufungua ofisi
za makao makuu Jijini Dodoma kwa kuwa ndiyo makao makuu ya serikali.
Wito
huo umetolea na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza,
alipotembelea ofisi ndogo za makao makuu ya Chama cha Wakulima (AAFP) jijini Dodoma
hivi karibuni.
Nyahoza
alisema kuwa Vyama vyote vya Siasa vinatakiwa kuwa na ofisi za makao makuu
jijini Dodoma kwa kuwa ndiko shughuli zote za serikali zinapofanyka kutokana na
serikali kuhamishia makao makuu yake jijini humo.
“Natoa
wito kwa vyama vingine vya siasa ambavyo havina ofisi ndogo za makao makuu
jijini Dodoma kufungua ofisi zao ukizingatia kuna vyama vya siasa ambavyo
vinapata ruzuku ya Serikali ninategemea viwe na ofisi bora na nzuri hapa Dodoma
kwa sababu uwezo huo wanao”, alisema Nyahoza.
Aliongeza
kuwa awali vyama vya siasa vilifungua ofisi zao jijini Dar es Salaam kwa kuwa
shughuli za kiserikali zilikuwa huko kabla ya kuhamishiwa Dodoma ambapo ndio makao
makuu.
“Kama
ambavyo mlienda kufungua ofisi za vyama vya siasa jijini Dar es Salaam kutokana
na kuwa karibu na ofisi za serikali, natoa wito sasa kwa vyama hivyo kuja
Dodoma na kufungua ofisi zao kwakuwa huku ndiko makao makuu ya nchi na Serikali”,
alisisitiza Nyahoza.
Katika
hatua nyingine Msajili huyo Msaidizi wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza, amevitaka
vyama vya siasa nchini kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na
maambukizi ya ugonjwa COVID -19 unaosambazwa na virusi vya Corona.
“Kuna vyama vingine sasa hivi vinajiandaa
kufanya mikutano mikuu ya kitaifa ya uchaguzi tunaomba hili jambo walizingatie
kabisa kama ikiwezeka waahirishe mikutano kuepuka kuleta mikusanyiko kinyume na
maelekezo ya Serikali badala yake wasogeze mbele mikutano hiyo.” Aliongeza
Nyahoza.
Ziara
hiyo ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutembelea ofisi ndogo za makao makuu
ya vyama vya siasa zilizoko makao makuu ya nchi jijini Dodoma ni muendelezo wa
zoezi wa uhakiki wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu lililoanza tarehe
17 Machi 2020.
Katika ziara hiyo vyama viliyotembelewa jijini Dodoma ni pamoja
na CCM, AAFP, NRA, CHADEMA, Demokrasia Makini na UMD.
No comments:
Post a Comment