April 22, 2020

WATANZANIA WENYE UWEZO WATAKIWA KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA

 Mkurugenzi wa Kiwanda cha Husseini Plastic Industries Ltd cha jijini Tanga, Yusuph Hassanali (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada matanki 5.
 Mkurugenzi wa Kiwanda cha Husseini Plastic Industries Limited cha Jijini Tanga, Yusuph Hassanali kulia akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto wakati wa makabidhiano ya msaada huo.
  Mkurugenzi wa Kiwanda cha Husseini Plastic Industries Limited cha Jijini Tanga, Yusuph Hassanali kulia akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto wakati wa makabidhiano ya msaada huo.

 
Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wenye uwezo wametakiwa kuwa mstari wa mbele kusaidia katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona kwa kutoa msaada mbalimbali itakayosaidia kukabiliana nao.

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Husseini Plastic Industries Limited cha Jijini Tanga, Yusuph Hassanali mara baada ya kukabidhi msaada wa matenki 5 yenye lita 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali kupambana na ugonjwa huo.

Alisema kwamba waliamua kutoa msaada huo baada ya kupita maeneo mbalimbali kuona kuna mkusanyiko wa watu kutokana na uwepo wa ndoo zenye lita 20 hivyo alipoona hali hiyo akaona upo umuhimu wa kuweza kutoa msaada huo.

Aidha alisema kwamba iwapo wakihitaji matenki mengine wameongeza kusaidia matenki ya lita hizo huku wakiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia juhudi za serikali kupambana na ugonjwa huo.

“Lakini pia niwatake watu wengine kulisaidia Taifa kwa kutoa msaada kwani ugonjwa huo umeleta athari kubwa kwa wananchi “Alisema

Hata hivyo alisema hivi sasa wao wameanza kuchukua tahadhari wakati wakiwahudumia wateja dukani kwao kwa kukaa umbali wa mita sita na hata kwenye eneo la biashara wana wahudumui wateja mmoja au wawili.

Mkurugenzi huyo aliwataka wakazi wa Mkoa wa Tanga wenye uwezo waweze kuwa mstari wa mbele na sio mpaka wasubirie waombwe badala yake wahamasike kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Corona

No comments:

Post a Comment

Pages