*Idadi ya wagonjwa yafikia
284, ataka tahadhari zaidi iongezwe
*Aomba viongozi wa dini wahakikishe
mikusanyiko ibadani inapungua
*Akemea wanaopandisha bei za
vyakula hasa sukari
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Alex Malasusa wa KKKT Jimbo
la Mashariki na Pwani (kushoto), Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la
Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi (wa pili kushoto), Mufti na Sheikh
Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zubeir (wa tatu kushoto) na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa nne
kushoto) katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa
wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. (PIcha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. Kushoto ni Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi na kulia ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. Kushoto ni Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi na kulia ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Dar es Salaam, Tanzania
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
hadi kufikia jana (Aprili 21, 2020) jumla ya wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na virusi vya
ugonjwa wa corona (Covid-19) ambapo wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, saba wako
kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki.
Ametoa kauli hiyo
leo (Jumatano, Aprili
22, 2020) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini walioshiriki maombezi ya
Kitaifa dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) yaliyofanyika kwenye
viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Amesema jumla
ya watu 2,815 waliokuwa karibu na wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati
yao, watu 1,733 walikutwa hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi
hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284).
“Shirika la
Afya Duniani lilikadiria kuwa ifikapo mwishoni wa Aprili, 2020 nchi yetu ingekuwa
na wagonjwa 524,716 lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa kadirio hilo
hatujalifikia.”
Kuhusu hali ya
maambukizi ilivyo nchini, Waziri Mkuu amesema Jiji la Dar es Saalam na kisiwa
cha Zanzibar, yanaongoza kwa maambukizi na akataka tahadhari zaidi zichukuliwe.
“Jiji la Dar es Salaam ndio lina maambukizi makubwa hivyo nawasihi wananchi
kama huna jambo lolote la kufanya huna sababu ya kuzurura na kwa
wafanyabiashara siyo lazima mje Kariakoo, unaweza kufanyia biashara katika eneo
lako,” amesisitiza.
“Ni
wakati kila mmoja kuendelea kuchukua tahadhari vya kutosha ili kuepuka
maambukizi. Epuka misongamano isiyokuwa ya lazima, huna sababu ya kumuamini
yeyote, ona kuwa kila mmoja ana ugonjwa.”
Kipekee, Waziri
Mkuu amewaomba viongozi wa dini waendelee kuchukua hatua madhubuti za kujikinga
na ugonjwa huo kwa kuwaelimisha waumini wachukue tahadhari zote muhimu. “Ninawaomba
viongozi wa dini wachukue tahadhari zaidi kwa kuhakikisha mikusanyiko kwenye
nyumba za ibada inapungua ikiwemo waumini kukakaa kwa nafasi, umbali wa angalau
mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine na kuweka maeneo ya kunawa kwa maji na
sabuni pamoja na vitakasa mikono katika nyumba zote za ibada.
“Kupunguza idadi
ya siku za kukutana kufanya ibada na masaa ya ibada au mahubiri kila inapobidi.
Kwa mfano, mikutano au shughuli za mikusanyiko za vikundi vya uimbaji, vijana, akinamama
au waumini kwa ujumla ni vema zikasitishwa katika kipindi hiki,” amesisitiza.
Kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Serikali, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuchukua
hatua mbalimbali za kudhibiti kuenea zaidi kwa ugonjwa huu zikiwemo za kutoa
elimu ya namna ya kujikinga, kuunda Kamati za Kitaifa kwa ngazi za Mawaziri,
Makatibu Wakuu, Timu ya Wataalam wa afya pamoja na kutoa maelekezo kwa Kamati
za Ulinzi na Usalama.
“Tumetenga
maeneo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huu,
tumenunua vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huu hususani kwa watoa huduma wa
afya. Tumeimarisha maabara zetu kwa lengo la kupanua wigo wa kufanikisha
upimaji wa sampuli, vituo zaidi ya saba nchini ambapo upimaji wa awali
unaanzia huko na kwenda kuhakikishwa katika Maabara Kuu ya Taifa,” amesema.
Wakati
huohuo, taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetaja
mikoa ambayo imepata wagonjwa wapya 30 kutoka idadi ya 254 iliyotangazwa mara
ya mwisho.
Wagonjwa hao na idadi yao
kwenye mabano wanatoka mikoa ya Dar es Salaam (10), Zanzibar (9), Mwanza (4), Pwani
(2), Dodoma (2). Mingine ni Kagera, Manyara na Morogoro ambayo yote ina mgonjwa
mmoja mmoja.
Katika
hatua nyingine,
Waziri Mkuu amekemea tabia ya baadhi
ya wafanyabiashara
wanaopenda kupandisha bei za vyakula wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
“Wiki hii
waumini wa Kiislamu wanaanza mfungo wa Ramadhan, hivyo natoa wito kwa
wafanyabiashara kuhakikisha vyakula muhimu katika kipindi hiki vinauzwa kwa bei
ya kawaida, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wafanye ukaguzi wa mara kwa mara kwenye
masoko ili kuhakikisha bei ni ile ile.”
Amesema kuwa hivi
sasa kuna sukari ya kutosha nchini hivyo bei itaendelea kuwa ileile bila kujali
msimu. “Ninaawagiza Wakuu wa Mikoa, yeyote atakayekutwa anauza sukari kwa bei ya
sh.4,500, chukua hatua dhidi yake kwani hayo si malengo ya Serikali yetu,”
amesisitiza.
Kwa upande wao, wakizungumza kwa nyakati tofauti,
viongozi wa dini walioshiriki maombi hayo, wameipongeza Serikali kwa hatua
ambazo imezichukua hadi sasa katika kukabiliana na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment