Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Denice Mwila, akipokea vifaa hivyo.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wilayani Misenyi mkoani Kagera Yasintha Simon amekabidhi vifaa mbali mbali vya kujikinga na ugonjwa wa Corona ili kuunga mkono jitihada za serikali dhidi ya janga hilo.
Akikabidhi vifaa vifaa hivyo ikiwemo ndoo 20 kwa ajili ya kunawia mikono, sabuni za chupa zitapatazo 20 katibu wa UVCCM wilayani Misenyi kwa niaba ya mwenyekiti wa umoja huo, katibu wa UVCCM Bwana Kadogo waziri amesema kuwa wao kama vijana wamewiwa kujitoa ili kusaidia jamii katika mapambano hayo kutokana na wilaya hiyo ya Misenyi kuwa na muingiliano mkubwa wa ki mipaka kutokana na wingi wa wananchi hasa raia kutoka nchini Uganda kuingia wilayani humo kwa kasi kubwa.
Bwana Waziri amesema umoja huo utaendelea kushirikiana na serikali kwani janga la Corona si mtu mmoja.
Akipokea vifaa hivyo mkuu wa wilaya ya Misenyi ameushukuru umoja huo wa kwa kujitoa huku akiwaomba viongozi mbali mbali wenye moyo wa kujitoa waendelee kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano hayo.
Hata hivyo vijana hao wameitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhali na kufuata maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

No comments:
Post a Comment