HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini hapa Bashe amebainisha kwamba
mikakati hiyo nipamoja na kuhakikisha wakulima wanapatiwa Pembejeo na
uhakika wa masomo kea njia ya minada.
"Nimekutana
na Vyama vya ushirika kwenye sekta ya Chai ili kuangalia changamoto
zinazowakabili lengo likiwa ni kuinua sekta hii muhimu kwa mustakabari
wa Maendeleo ya wakulima wetu na viwanda vya kuchakata chai kwa ujumla,"
amesema Bashe.
Aidha
amesema katika kikao hicho wameweza kujadaili mfumo wanaotumia wakulima
kupata Pembejeo ambapo aliwataka wakulima wote nchini kuagiza mbolea
kupitia Vyama vyao vya Ushirika iliwaweze kupata kwa punguzo la bei pia
kwa mikopo.
"Mwaka jana
tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini mwaka huu tunataka tufanya zaidi
angalia kila mkulima apate mbolea kupitia mfumo wa kuchukua mbolea
halafu unalipa baada ya siku 180 ambapo katika muda huo Kila mkulima
atakuwa amevuna mazao yake inakuwa rahisi kulipa"anaeleza Bashe
Kwa Upande wake Mkurugenzi kutoka Bodi ya Chai Tanzania Nicholaus Mauye
Amesema lengo la kikao hicho ni kuona Maendeleo ya tansinia kupitia mkulima mdogo mdogo wa chai
Amesema
Katika kikao hicho changamoto za wakulima na mikakati yao imechukuliwa
na kwenda kufanyia kazi ili kukifanya Kilimo cha chai kinakuwa chenye
tika kwa wakulima.
Naye
Meneja wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja Maduhu Mkonya amesema wamekutana
wakulima hao kuhakikisha wanapata mbolea kwa kuagiza kupitia mfumo huo
wa Kilektronik ambao fedha zake mkulima analipa kwa muda wa miezi 6
baada ya kuvuna mazao yake.
Amesema
mfumo huo ni kama huba kwani unaendeshwa kwa njia ya Kilektronik ambapo
suala la kuchelewa au mbolea kuulizwa kwa bei ya juu haitakuwepo.
Naye
Mkulima Santino Mtenda mkulima wa chai na mkonge kutoka Wilaya ya
Mufindi Mkoani Iringa Amesema zao la chai ni zao la kimkakati hivyo
wamepata faraja baada ya kuona Serikali inaanzisha minada kwani masomo
kwa wakulima yataimalika.



No comments:
Post a Comment