HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 23, 2021

HARAMBEE YA UJENZI WA SEKONDARI YA BI. TITI MOHAMED

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Lt. Col Patrick Sawala.

Hayati Bibi Titi Mohamed.

 

NA MWANDISHI WETU


WATANZANIA mbalimbali wamealikwa kujitokeza kuchangia ujenzi wa shule maalum ya Sekondari itakayoitwa Bi.Titi Mohamed kwa ajili ya kumuenzi mpigania Uhuru Mwanamama ambaye pia alikuwa mbunge wa kwanza Jimbo la Rufiji.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Umma ya mwaliko huo iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Lt. Col Patrick Sawala imeeleza kuwa:

"Tunawaalika wadau na watu mbalimbali kujitokeza kwenye Harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Sekondari Bi. Titi Mohamed, 27 February kuanzia majira ya Sita mchana hadi Saa 12 jioni Katika Ukumbi wa SabaSaba ndani ya viwanja vya Sabasaba, barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam"  Ilieleza taarifa hiyo.

Aidha, mchango wa Harambee pia wadau na Wananchi wanaweza kuutuma kupitia: Benki ya NMB yenye jina la Maendeleo Kata ya Ngorongo akaunti namba 21310024867.

Pia michango inaweza kutumwa kwa njia ya mtandao wa simu wa Tigo Pesa namba 0716480956 yenye jina la Sikujua Gallusy Mavika". alieleza mkuu wa Wilaya kwenye taarifa hiyo. 

 Aidha shule hiyo inatarajiwa kujengwa kwa nguvu za Wananchi, wadau  wa Maendeleo, na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji hili ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano katika kuhakikisha kila mtoto mwenye sifa ya kwenda shule anaenda shule bila kikwazo na bila malipo yoyote.

Akifafanua zaidi, alisema ghalama za awali kwenye ujenzi wa shule hiyo ni  zaidi ya Tshs Milioni  550. Hivyo  wanatarajia kukusanya Tshs. Bilioni moja ilikukamilisha ujenzi wake kiujumla.

Hata hivyo wananchi na Wadau wanaweza pia kuchangia fedha taslimu au vifaa vya ujenzi moja kwa moja kwa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Rufiji. 

Katika tukio hilo, wadau mbali mbali wakiwemo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Serikali na wageni waalikwa watashiriki.

No comments:

Post a Comment

Pages