HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2021

MKAZI WA KAGERA ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMUUA MAMA YAKE MZAZI

 


Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Kagera Revocatus Malini. 

 

 Na Lydia Lugakila, Kagera

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Fredius Philbart Kibengo mkazi wa eneo la Omurushaka wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua  mama yake mzazi kwa kumkata shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali baada ya Mganga wa kienyeji kumtaka kupeleka damu ya mama yake au ndugu yake wa karibu ili kutengenezewa dawa za kuongeza utajiri kwenye biashara.

Katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi Mkoani Kagera limebaini kuwa kabla tukio hilo kutokea mtuhumiwa alisafiri kuelekea nchini Burundi kutafuta dawa za kuongeza utajiri na alipo rejea nyumbani kwakwe alimshirikisha mke wake kuhusu sharti hilo alilopewa na Mganga wa kienyeji lakini mke wake hakukubaliana  na masharti hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Kagera Revocatus Malini, amesema Februari 17, 2021 mtuhumiwa alionekana maeneo ya nyumbani kwa mama yake mzazi na alipofika usiku wa kuamkia Februari 18,2021 alimvamia mama yake na kumkata na kitu chenye ncha Kali Kisha kuipoteza maisha.

Hata hivyo kamanda wa polisi Mkoani humo amewataka wananchi Mkoani Kagera kujiepusha na vitendo vya imani za kushirikiana  ambazo zimekuwa zikichangia
Mauaji ya watu wasio na hatia.

No comments:

Post a Comment

Pages