HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 02, 2021

NAIBU WAZIRI AZINDUA MRADI WA MAJI GERA MKOANI KAGERA


Naibu Waziri wa Maji, Merry Prisca Mahundi, akimtua ndoo kichwani mkazi wa Misenyi wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi ya maji Gera.

 

Naibu Waziri wa Maji Merry Prisca Mahundi amefanya uzinduzi wa awali wa Mradi wa Maji Gera utakaokamilika tarehe 15.3.2021  kwa kuwatua akina mama ndoo kichwani.

Naibu Waziri amefanya zoezi hilo wakati wa ziara yake ya siku moja Wilayani Missenyi aliyofanya kwa ajili yakukagua utekelezaji wa Mradi wa Maji Gera wenye thamani ya shilingi milioni 570 na Mradi wa Maji Kyaka Bunazi wenye thamani ya shilingi bilioni 15.1.

Akiwa Gera amewataka wananchi kutunza miundombinu ya Mradi huo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho nakwamba furaha ya Serikali nikuona wananchi wake wanapata Maji Safi na salama katika mabomba yaliyokaribu na makazi yao.

Akiwa Kyaka amewahakikishia wananchi kwamba Mradi huo utakamilika ndani ya muda Kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alivyoagiza wakati akiongea na Wananchi Kyaka Wilayani Missenyi mwezi Januari mwaka huu.

Naibu Waziri pia amesema baada ya Mradi huo utakaohudumia wananchi wa Mji mdogo wa Kyaka Bunazi kukamilika Serikali itahakikisha inauoanua ili kuwezesha wananchi wa Kata za jirani Nsunga na Mutukula wanapata Maji ya bomba kutoka Mto Kagera.

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Nkenge Florent Kyombo amempongeza naibu Waziri kwakutelekeza ahadi yake aliyotoa Bungeni Dodoma yakukagua Mradi pia akaishauri Wizara kutoa fedha kwa wakati ili kuwezesha Mkandarasi na Mamlaka ya Maji Mwanza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment

Pages