HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 02, 2021

SERIKALI NA TCRA KUWAONDOLEA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA MAWASILIANO WANANCHI WA VIJIJI VYA CHALINZE BAGAMOYO


Naibu Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari, Mhandisi  Adrea Kundo (katikati) akiwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Chalinze kwa juhudi zao za kuweza kukamilisha ujenzi wa jengo jipya  la halmashauri hiyo.

 

 

NA VICTOR  MASANGU, CHALINZE 

 

 NAIBU waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Mhandisi  Adrea  Kundo  ameyaagiza makampuni mbali mbali ya simu kuhakikisha kwamba wanaweka mipango ya kufanya utafiti wa kina katika maeneo  ambayo tayari yameweka uwekezaji wa kufunga mitambo yao ya minara  ili kuweza kubaini uhitaji wa matumizi ya wananchi  lengo ikiwa ni kuwaondolea adha na usumbufu wa ukosefu wa mawasiliano.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri ya Chalinze iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwai kwa ajili ya kuzungumza na watumishi pamoja na mamlaka zinazohusika na mawasiliano ili kuweza kujadili changamoto mbali mbali zilizopo na kuzifanyia kazi na kubioresha zaidi sekta ya mawasiliano.

Naibu Waziri huyo alisema kwamba nia kubwa ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kwamba inaborsha zaidi sekta ya mawasiliano katika maeneo mbali mbali hapa nchini hivyo ni vema wadau wa masuala hayo wanapaswa kuweka mikakati yao madhubuti ambayo itasaidia kuboresha mitambo yao ambayo wanaifunga ikiwemo  kwenda kuiangalia na kuifanyia ukarabati mara kwa mara ili iweze kufanya kazi vizuri kulingana na mahitaji ya wananchi.

 

“Hapa kitu kikubwa napenda kuagiza kwamba makampuni haya ya simu inatakiwa sasa kuhakikisha wanafanya uwekezaji waao ambao unatija na kuwafikia wananchi katika maeneo husika lakii kikubwa zaidi ni kufanya utafiti wa maeneo husika hasa ili kutembelea minara amabayo inakuwa imefungwa kwa kipindi cha muda mrefu, lakini kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watuamiaji mitambo inashindwa kuwafikia na wananchi katika maeneo mengine kwa hivyo ili ninaliomba sana,”aliongeza Naubi Waziri huyo.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa juhudi mbali mbali amabzo inazifanya lakini amebainisha kwamba bado kuna baadhi ya vijiji katika jimbo lake kuna chanagamoto ya  upatikanaji wa mawasilano ya  mtandao hivyo wananchi wanapata shida sana katika  suala zima la kuwasiliana.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Chalinze Ramadhani Posi waliongeza kuwa  kumekuwepo na baadhi ya  madhara yatokanayo na ukosefu wa mawasiliano hasa  pindi kunapoibuka  sakata la migogoro ya wakulima na wafugaji inakuwa ni chanagmto kupata taarifa kwa wakati na kuomba waongezewe ruzuku katika suala zima la mawasialino.

Kwa upande wake Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano TCRA Kanda ya Mashariki Mhandisi  Lawi Odiero  amebainisha kwamba lengo ambalo wamejiwekea ni kuhakikisha wanalinda na kuboresha sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo mbali mbali ambayo imetolewa inafutwa bilaya kuvunjwa nia ikiwa ni kuhakikisha kwamba huduma na hiyo inaleta mabadiliko chanya.

 

“Kwa sasa mabadiliko katika sekta hii kwa kweli yameleta mabadiliko makubwa sana na kuweza kurahisiha na kubadili hata kasi ya maendeleo kutokana na kuendesha na kufanya shughui zetu za kuwasiliana hivyo kumesaidia kuongeza tija zaidi katika mambo mengine hata ya kubadilisha kasi ya maendeleo kwa wananchi wetu wa Tanzania,”alibainisha Mhandisi Odiero.

Kadhalika aliongeza kuwa kwa sasa TCRA kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa vyombo vya habari itawasaidia kwa hali na mali katika kuwapa miongozo ambayo itawasaidia kufungua redio mbalimbali za kijamiii ambazo zitakuwa zikitumika katika kuwafikishia ujumbe juu ya shughuli za kimaendeleo amabzo zinafanyika katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment

Pages