April 22, 2021

Waitara atema Cheche

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mwita Waitara ameagiza wakala wa Ufundi na Umeme nchini TEMESA kuhakikisha wanafanya kazi kwa faida itakayowawezesha kutoa gawio serikalini bila kushinikizwa.


Naibu Waziriaziri Waitara ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akizungumza na menejimenti ya TEMESA mara baada ya kutembelea na kukagua karakana ambapo amesema ili kuifanya serikali iwe na nguvu ni lazima Taasisi zake zijiendeshe kwa faida.
 
Hata hivyo amewataka wakala hao kuhakikisha kuwa magari na mitambo ya serikali inayohitaji matengenezo katika karakana za TEMESA kote nchini yanashughulikiwa kwa haraka.

Pia amewataka kupunguza bei ya utungenezaji wa magari ili Wateja  wasikimbie na kwenda kutengeneza kwenye makampuni mengine.

"Naagiza kwa magari na mitambo iliyotelekezwa katika karakana hii kuyaondoa haraka ili kuyapa nafasi magari mengine  yanayohiji kutengenezwa ndani ya  karakana hii,"amesema Waitara

Hata hivyo amesema TEMESA  ni 
Taasisi kubwa na ipo karibu kila Mikoa malalamiko yaliyopo  kuwa na bei kubwa ya matengenezo,magari kuchelewa na Spea kuuzwa kwa bei  kubwa na ndio Maana wataalamu wa TEMESA wanatoka nje na kwenda kufanya mazungumzo na Wateja ili wawatengenezee kwa bei nafuu.

"Naomba tuwaangalie wataalamu wetu utakuta mtu ni muajiriwa wa TEMESA halafu anachukuwa utaalamu wetu anachepuka na kwenda nje kutengeneza magari kwa kutumia Vifaa vya Taasisi yetu ya  TEMESA tabia hii naomba iachwe mara moja ," amesema 

Na kuongeza kuwa" Tukikugundua tutakushitaki kwa maana unatuibia,kama wewe una utaalam ,maoni  na mawazo yako peleka kwenye vikao vyenu vya Menejimenti  na huyo anaeona huko nje ndio kunamanufaa zaidi atoe maoni hapa halifu nyie muyachakate maoni hayo na mkubaliane yale mnayoona yana manufaa kwenu yafanyeni na kama mkishindwa kuna Wizara tutawapa ushirikiano wa kutosha ili kuboresha Taasisi hii"ameongeza Waziri

Awali taarifa ya mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme TEMESA Mhandisi Japhet Maselle imebainisha majukumu ya wakala kwa kipindi cha mwaka wa fedha unaomalizika ikiwamo utekelezaji wa miradi 35 iliyogawanyika katika makundi manne ambayo ni ujenzi, ununuzi, ujenzi na ukarabati wa maegesho ya vivuko pamoja na ujenzi wa karakana.


No comments:

Post a Comment

Pages