HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 28, 2022

TUWE NA UTAMADUNI WA KUPANDA MITI-DK. MNDOLWA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa Dkt Edmund Mndolwa ameitaka jamii kuwa na utamaduni wa kupenda na kutunza mazingira huku akiendelea kutoa rai ya kuacha kukata miti hovyo ili kuondokana na tatizo kubwa  la mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo amesasema jijini Dodoma wakati wa zoezi la kufanya usafi katika soko Kuu la Majengo na upandaji wa miti kwenye shule ya Msingi ya Dodoma Mlimani wakati wa madhimisha miaka 45 ya jumuia ya wazazi.

Amesema nchi ya Tanzania imekuwa kwenye changamoto kubwa ya kukosa mvua yote ni kutokana kutotunza mazingira.

"Hali ya usafi na uhifadhi mazingira katika nchi yetu sio nzuri kama tunavyojionea hapa kwenye hili soko limejaa Kumekuwa na ongezeko kubwa la taka zinazotoka majumbani hosptali na masokoni hivyo ukiona taka hizo toa taarifa sehemu usika ," amesema.

Aidha amesema, utafiti unaonyesha kuwa hekta laki 4 za miti zinakatwa Tanzania kila mwaka ambapo ameeleza kama hali hiyo haitakemewa na kuachwa kuendelea hivyo basi nchi  itaishia kuwa jangwa .

"Zamani tulikuwa na msemo unaosema  ukikata mti panda mti sasa sisi kama jumuiya ya wazazi tuanasema ukikata miti panda miti mingi," amesema Mwenyewe kiti huyo

Sambamba na hilo amebainisha kwamba,Jumuiya ya wazazi wapo katika mpamgo wa kuzungumza na Serikali na ili waweke mpango wa kupanda miti milioni 200 na zaidi.

 "Ni kweli namba ya miti ni iko juu na mnaweza kuwaza kuwa  kulitimiza hilo ni jambo gumu lakini ninahakika tutatimiza kwa kila kaya kupanda miti mitano na kila wilaya kuwa  na kitaru tutakuwa nchi yetu itakuwa na miti ya kutosha," smesema

No comments:

Post a Comment

Pages