Na Mwandishi Wetu, Simiyu
MKUU
wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulika amevunja Vyama vya Ushirika (AMCOS),
335 na kufukuzwa maofisa ushirika watano kwa kushindwa kutekeleza
majukumu yao ipasavyo.
Aidha, Kafulila amesema mkoa huo umejipanga kuhakikisha bei ya zao la
Pamba inavunja rekodi ya miaka 30, huku wakianisha mambo tisa ya kuhusu mwelekeo wa zao hilo.
Kafulila
amechukua uamuzi huo wakuwatimua na kuvunja uongozi wakati wa kikao cha
mafunzo ya usimamizi wa ununuzi wa pamba msimu huu kilichofanyika
wilayani Bariadi mkoani humo.
Amesema
zao maofisa na viongozi wa AMCOS wameshindwa kusimamia majukumu yao
ipasavyo hivyo ni vema wakapisha sura mpya ambazo zitaendana na kasi ya
mkoa.
"Inafahamika
Simiyu ndio Simba wa Pamba Tanzania ikizalisha wastani wa asilimia 40
hadi 60. Pamoja na bei nzuri msimu uliopita kufikia Sh.1800, bado kuna
malalamiko mengi yaliyothibitika mchezo mchafu kati ya AMCOS na Maofisa
Ushirika uliosababisha mkulima kutopata bei halisi iliyolipwa na
mnunuzi" alisisitiza RC Kafulila.
Aidha
Kafulila amesema pamoja na kuwasimamisha kazi maofisa ushirika watano
na kuvunja uongozi wa AMCOS, pia ameitaka PCCB kufanya uchunguzi
imkuhakiki kila AMCOS ili kuona vielelezo na kuthibitisha malipo
aliyolipwa mkulima na kiasi ambacho AMCOS iliuza pamba kwa niaba ya
mkulima.
Amesema mpaka sasa zimechunguzwa AMCOS 189 na zote hakuna vielelezo kuthibitisha malipo sahihi kwa mkulima.
RC
Kafulila amesema kwa kuzingatia changamoto hizo na zaidi maelekezo ya
Rais Samia Suluhu Hassan kutaka kusafisha mfumo mzima wa usimamizi zao
la pamba hasa katika msimu huu ambao makadirio ya Bodi ya Pamba
yanaonesha Simiyu itavuna zaidi ya mara tatu ya msimu uliokwisha kwa
kupata kati ya tani 250,000 mpaka 300,000.
Amesema kiasi hicho cha Pamba kinachotarajiwa kuvunwa hakijawahi kupatikana hata ukiunganisha na Mkoa wa Shinyanga.
Kafulila
ameeleza mwelekeo mpya wa usimamizi wa manunuzi ya Pamba msimu huu
unaonza Mei 20, 2022 ni kui imarisha uwajibikaji wa AMCOS kwa
kuhakikisha AMCOS zote zinafutwa na hivyo uchaguzi utarudiwa ndani ya
wiki Moja.
"Pili, ili
kuhakikisha uchaguzi huo unaleta viongozi thabiti, wakulima wote wa
pamba kwenye kijiji husika watakuwa na haki ya kushiriki uchaguzi. Hii
inatokana na ukweli kuwa wanachama wa AMCOS hawazidi asilimia 30 ya
wakulima wote.
Hivyo
asilimia 70 ya wakulima ambao sio wanachama wa AMCOS washiriki uchaguzi
huo. Haki hii pia inachangiwa na ukweli kwamba AMCOS zinalipwa shilingi
kwa kila kilo ya Pamba bila kujali ni ya mwanachama au asiye mwanachama
wa ushirika.
Mkuu wa mkoa
huo alisema, ili kuongeza uwazi, wakati wa manunuzi msimu huu unaoanza
Mei 20, 2022, kila AMCOS itapaswa kuweka wazi kwenye kituo cha manunuzi
bei ya kila mnunuzi aliyewapa pesa wamnunulie pamba, ili wanunuzi
watakaonunua pamba kupitia AMCOS wajue kwanini wanapata au wanakosa
kulingana na bei zao wanazotaka AMCOS iwanunulie pamba.
"Nne,
ili kuhakikisha usimamizi thabiti, Kafulila amelekeza wakurugenzi
Halmashauri Bariadi Mjini, Vijijini, Maswa, Busega, Itilima na Meatu
kuwaondoa maofisa ushirika wote ngazi ya wilaya na kupangiwa kazi
zingine na taratibu za kuweka maofisa wengine zifanyike ndani ya wiki
moja.
Tano, ili kuongeza
uwazi na ushindani wanunuzi binafsi wataruhusiwa kuweka mawakala wao
kwenye soko la pamba na kushindana na AMCOS katika masoko hayo vijijini
na wote AMCOS na mawakala wanunuzi watasimamiwa na Serikali ya kijiji
chini ya mtendaji wa kijiji,"amesema.
Amesema mtendaji wa kijiji ndio msimamizi mkuu wa uuzaji wa pamba akishirikiana na AMCOS.
RC
Kafulila amesema jambo la sita, ili kuhakikisha usimamizi thabiti,
pamba yoyote halali itapaswa kuwa na iliyouzwa kwa bei sawa au zaidi ya
bei elekezi na iwe na kibali kilichothibitishwa na mtendaji wa kijiji na
AMCOS pamba iliponunuliwa
Aidha, Kafulila amesema ili kuongeza ufanisi makatibu wa AMCOS watapaswa kutoka ndani ya kata husika.
Kwa
upande mwingine amesema mkulima atakuwa na uhuru wa kuuza Pamba kwa
AMCOS au wakala wa mnunuzi binafsi ambao wote watakuwa kwenye soko la
pamba chini ya mtendaji wa kijiji.
"Tisa,
wanunuzi wa Pamba watakuwa na uhuru wa kununua pamba kupitia AMCOS au
wakala wake lakini manunuzi yote yatasimamiwa na Serikali ya kijiji.
Wote, AMCOS na wakala wa mnunuzi watanunua Pamba kwenye soko ndani ya
kijiji na VEO atakuwa na msimamizi mkuu,"amesema.
Kafulila
amesema anawatakia wakulima na wananchi wote kutoa ushirikiano hasa
ikizingatiwa kuwa usimamizi thabiti wa Serikali utaendelea kuhakikisha
mkulima anapata bei nzuri.
"Nimeshiriki
kikao cha wataalamu wa Bodi ya pamba, Ushirika na Wanunuzi wa pamba
msimu huu kwa lengo la kuhakikisha mkulima anapata bei inayofanana na
jasho lake. Najua Waziri atatangaza bei elekezi Mei 20, lakini nachoweza
kuwahikishia wakulima ni kwamba bei itakuwa nzuri kuliko miaka yote
katika kumbukumbu za pamba tangu mwaka 1990," alihitimisha ndugu
Kafulila.
No comments:
Post a Comment