HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 10, 2023

AKAUNTI PEPE (VIRTUAL WALLET) YAZINDULIWA

Na Magrethy Katengu

KAMPUNI ya Simu ya TTCL imezindua huduma ya mpya ya akaunt pepe(virtual wallet) ambayo itawarahisishia wateja wa mtandao huo kupata huduma mbalimbali za malipo kwa kutoa na kutuma benki  yote popote walipo .

Akizungumza   leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde katika Maonyesho ya bishara sabasaba amesema huduma hiyo   ya Akaunti pepe (Virtual wallet)  ili kuwarahisishia wateja wao kufanya huduma mbalimbali kwa haraka zaidi.

“Kampuni ya T-PESA imeendelea kujikita kidigitali zaidi kwa kuzindua leo huduma ya . Huu ni mfumo rahisi wenye ufanisi kwa wateja wanaotumia huduma za kibenki kupitia simu  T-PESA," amesema"  Mkurugenzi huyo wa T-PESA.

Hata hivyo amesema  kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kufanya malipo mbalimbali popote walipo na kwa haraka zaidi, ikiwemo kulipia bili za maji, umeme, ving’amuzi na faini mbalimbali za Serikali.

Hata hivyo  amebainisha kuwa huduma hiyo inaenda kuwarahisishia kazi mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwani sasa kwa kutumia akaunt pepe wataweza kulipia viingiio vya mechi mbalimbali za mpira kwa NCARD.

"Huduma ya QR Code ni njia ya haraka na rahisi ya kufanya malipo ambayo  inawezekana katika maduka, migahawa na maeneo mbali mbali nchini ikiwemo vituo vya petrol vya Puma. Wateja pia wanaweza kuangalia salio bure ukiwa na bando la intanet  kununua au kutuma muda wa maongezi," amesema.

Watanzania na Wateja kwa ujumla waneshauriwa  kuendelea kutumia huduma za T-Pesa na kama bado hawana laini za TTCL basi wajisajili mara moja ili kufurahia huduma kwa bei nafuu.

"Huduma hii ya inapatikana kwenye ANDROID kwa kupakua kupitia google playstore Tunajivunia huduma hii kwani  ni tofauti na APP nyingine za mitandao ya simu kwa sababu ina huduma ya kipekee ya kumuwezesha mteja wetu kupata taarifa zake " aliongeza Bi. Mkudde.

Amesema Kampuni ya T-PESA itaendelea kuja na ubunifu mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta mbalimbali ili kuondoa changamoto zilizopo na kuendana na matumizi ya mifumo ya kidigitali na kupelekea upatikanaji wa huduma zake kwa wakati na urahisi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages