HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2023

FONDOH AGAWANYA 'BAHARI' AKITUA SIMBA SC

Na John Richard Marwa


HATIMAYE yule aliyetajwa kuigawanya bahari ya Hindi ametua kwa nyekundu na nyeupe. Mlinzi wa kimataifa wa Cameroon Che Fondoh Malone ametambulishwa Msimbazi.



Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba kupitia jukwaa lao la kidijitali imeeleza kuwa mlinzi huyo atawatumikia wekundu wa Msimbazi kwa misimu miwili ijayo.


"Uongozi wa Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kumsajili mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone (24) raia wa Cameroon kutoka Cotton Sports FC kwa mkataba wa miaka miwili.  

"Che Malone amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Cotton Sports kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Cameroon msimu uliopita akiwa nahodha huku akicheza karibia mechi zote." Imeeleza taarifa hiyo na kubainisha kuwa.

"Che Malone ambaye anajulikana kwa jina la utani 'Ukuta wa Yericko' ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Cameroon (MVP) msimu wa 20222/23.

"Che Malone ameitwa kwenye kikosi cha timu Taifa ya Cameroon 'Indomitable Lions' pamoja na timu inayoshiriki michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

"Che Malone ni mchezaji mwenye uzoefu wa kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Shirikisho hivyo tunaamini atakuwa msaada mkubwa kikosini.

Che Malone anatua Msimbazi kuchukua nafasi ya Joash Onyango ambaye siku mbili zilizopita alijiunga na Singida Fountain Gate FC kwa mkopo wa msimu mmoja. Huku Malone anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Mnyama katika dirisha hili la usajili baada ya Willy Essomba Onana na Aubin Kramo Kouame.


No comments:

Post a Comment

Pages