HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2023

Marais Watatu Wastaafu wa Afrika Kushiriki Mkutano wa Demokrasia Arusha Julai 17

Marais watatu wastaafu kutoka Afrika wanatarajiwa kushiriki mkutano mkubwa wa mwaka unaoangazia masuala ya uongozi na demokrasia barani Afrika unaotegemewa kufanyika jijini Arusha kwa siku tatu kuanzia Julai 19 mpaka Julai 21, 2023. 

 

Ukijulikana kwa kimombo kama Africa Drive for Democracy, mkutano huo utatatanguliwa na kikao cha viongozi mashuhuri wastaafu kuhusu hali ya demokrasia barani Afrika kitakachofanyika kati ya Julai 17 na Julai 18, 2023, katika ukumbi wa hoteli ya Gran Melia, huku Rais Samia Suluhu Hassan akitegemewa kuwa mgeni wake rasmi. 

 

Marais wastaafu watakaoshiriki katika kikao hiki ni pamoja na Jakaya Kikwete (Tanzania), Ernest Bai (Sierra Leone) na Joaquim Chissano (Msumbiji). Pia, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, anategemewa kushiriki kwenye kikao hicho. 

 

Kikao hicho kitafuatiwa na mkutano mkubwa kuhusu hatma ya demokrasia barani Afrika utakaofanyika kuanzia Julai 19 mpaka Julai 21, 2023, katika ukumbi wa MS-TCDC Usa River, Arusha.  

 

Kwa mujibu wa waandaji wa mkutano huo – MS-TCDC (Tanzania), Center for Strategic Litigation (Tanzania), na Institute for Security Studies (Afrika Kusini) – washiriki takribani 200 kutoka nchi mbalimbali za Afrika watashiriki kwenye mkutano huo ili kujadili kwa pamoja maendeleo ya demokrasia katika bara la Afrika. 

 

Waandaaji wa mkutano huu wamewaalika waandishi wa habari kushiriki hafla ya ufunguzi wa kikao cha viongozi mashuhuri hapo Julai 17, 2023. Pia, waandaaji wa mkutano huo wamepanga kufanya mkutano na wanahabari hapo Julai 18, 2023, kuanzia saa sita mchana kuhusu mkutano huo.



No comments:

Post a Comment

Pages