HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 11, 2023

SERIKALI KUENDELEA KUFANYIA MABORESHO SEKTA YA MICHEZO ILI KUSAIDIA LUGHA YA KISWAHILI KUJULIKANA KIMATAIFA

Waziri Balozi Pindi Chana akitumbuiza mwenywe na kupiga gitaa mwenyewe Mambo ya Sabasaba hayo Banda la Wizara ya Tamaduni Sanaa na Michezo.


Na Magrethy Katengu


Waziri wa Tamaduni Sanaa na Michezo Balozi Pindi Chana Sekta ya michezo amesema Serikali inaendelea na jitihaza za kuhakikisha maboresho yanafanyika hasa sekta ya michezo kwani kwani ndiyo chachu inayosaidia lugha ya Kiswahili kuenea na kutumika  Duniani kote


Akizungumza leo Jijini Dar es salaam wakati alipotembelea Maonyesho ya Biashara sabasaba ambapo amesema Sasa Wasanii wa muziki,waigizaji wa filamu na wapenda soka wamejionea wenyewe namna Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan anavyounga mkono kusaidia vijana wenye vipaji hivyo waendelee kufanya vizuri akitolea mfano wa Mpoki,na Sholo Mwamba walivyokwenda nchi nyingine kutoa burudani hivyo inaonyesha jinsi sanaa inavyokuwa


"Elimu inaendelea kutolewa katika banda la Wizara Tamaduni Sanaa na Michezo sabasaba  na wananchi wanakaribishwa kupata elimu ya masuala mbalimbali watajionea kazi za wasanii wa kale zilivyokuwa zinayengenezwa na  zilizohifadhiwa zinaonyesha wapi tulipotoka na wapi tunapokwenda kiteknolojia kuweza kufanya kazi za sanaa vizuri zaidi" amesema Balozi Chana


 Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa Rais Dkt Samia Suluh Hassan amekuwa mstari wa mbele kuunga mkono  timu zote za mpira wa miguu  kwa kutoa kiasi cha fedha kuanzia shilingi milioni tano timu itakayoifunga timu iliyotoka nje ya nchi pia sasa timu ya Taifa ya mpira wa miguu kocha wake mpya analipwa na serikali hii inaonyesha nia yake ya dhati kupenda michezo . 


Sanjari na hayo amebainisha kuwa amepokea vifaa vya michezo kutoka Ubalozi wa China hivyo Watahakikisha vinafika kila Mkoa nchini hivyo kutumika katika mlengo uliokusudiwa 


Pia amesa kuwa Rais kwa upande Utamaduni na Sanaa amekuwa jirani na Machifu wa nchi nzima na yeye ndiye Chifu Mkuu anayetambulika kwa jina la Hangaya hii inaonyesha dhamira yake ya kupenda sanaa na tamaduni ya nchi yake.


"Tumeshuhudia vikundi vya Mziki vikipata mialiko ya kwenda nje ya nchi hivyo kupitia wao mziki wetu  Sanaa na tamaduni yetu inazidi kujulikana katika mataifa mbalimbali na lugha ya kiswahili sasa imekuwa ikitumika katika vikao vya Afrika hii ni kuonesha Kiswahili kikishika nafasi"amesema Balozi Chana


Aidha Wizara ya Utamaduni sanaa na Michezo itaendelea kuratibu kupatikana kwa waalimu na wakalimani wa lugha ya kiswahili kwenda kukifundisha nchi mbalimbali kwani  ngazi ya umoja wa Mataifa imetambua kiswahili kuwa lugha ya kwanza na kutengewa siku yake maalumu ya kuidhimisha kimataifa

No comments:

Post a Comment

Pages