HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2023

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE YAIBUKA KINARA TUZO, MAONESHO YA SABASABA


Na John Marwa

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) imetwaa tuzo ya mshindi wa jumla katika maonesho ya Biashara ya kimataifa ya Sabasaba ambayo yamefika tamati hapo jana.

Hayo yamebainishwa na Dk. Peter Kisenge, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC).

"Tumefarijika sana katika maonesho haya ya Sabasaba ambayo ni maadhimisho ya 47 ya Biashara. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa mshindi wa kwanza kwa ujumla, kama unavyojua yapo mashirika zaidi ya miamoja yameshiriki na sisi tumekuwa washindi wa kwanza kwa ujumla.

"Vilevile tumepata tuzo nyingine kwa kuwa mshindi wa kwanza katika kundi la Afya pamoja na vifaa tiba, kwa sababu gani tuumeweza kushinda?, Hii imechochewa na kuwa na wafanyakazi wenye ueledi mkubwa sana na wafanyakazi wenye ujuzi mkubwa wa kutoa huduma kwa wateja ambayo ina viwango vya kimataifa." Amesema na kuongeza kuwa.

"Wafanyakazi wa Jakaya Kikwete wameonyesha ueledi mkubwa sana, watu wengi walikuwa wanakuja kwenye Banda letu kupata huduma, Lakini tulikuwa na vifaa mbalimbali vya kuchunguza magonjwa ya Moyo, tuliweza kuonyesha huduma ya upasuaji wa Moyo ambayo tunaifanya lakini tuliweza kuonyesha huduma ambayo tunaitoa Sasa hivi ya tiba utalii ambapo karibu ya nchi 20 zinakuja kwenye Taasisi yetu kuweza kupata huduma mbalimbali.


"Tumeweza kutoa vilevile huduma ya haraka kwa mgonjwa ambaye amezidiwa gafla, ambapo kama ukipata mshtuko ghafla wa Moyo unaweza kuja kwenye Taasisi yetu.

"Vilevile tumetoa Elimu ya kujilinda na malazi ya Moyo ambayo watu wengi walikuwa wamekuja kupata, kwaiyo kwa nini tumeweza kushinda ni kwa sababu ya hayo yote ambayo nimewaeleza.

"Lakini yote hayo ni kwa sababu ya uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Serikali yetu ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu, kwa sababu kuna uwekezaji mkubwa sana kwenye Taasisi yetu ambao umefanywa wa vifaa tiba, vimewekwa pale kama vifaa vya upasuaji vikiwa na gharama zaidi ya ma Billion ya pesa ambayo yamewekezwa na Serikali." Dk. Peter Kisenge amebainisha kuwa.

"Nadhani hizi ndio sababu zimechochea sisi kushinda katika maadhimisho haya ya Sabasaba." Amesema Dr Peter Richard Kusenge huku akitoa ushauri kwa Wananchi.

"Niwashauri Wananchi wapende kupima afya zao kwa kuchunguza haya magonjwa ya Moyo lakini wafanye mazoezi, wajitaidi wanapokuwa wanakula vyakula vya wanga sana vinaweza kuchochea uzito, kwaiyo waweze kujiokoa na hayo mambo, vilevile waache uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe."

No comments:

Post a Comment

Pages