Waziri
wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ameshudia uwekaji
wa saini mikataba ya makampuni kumi wenye hadhi ya uwekezaji wa
kimkakati mahiri wenye jumla ya thamani ya Dola za Marekani Mil
1805.12 na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Katika
uwekezaji huo uliopewa hadhi hiyo na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji
(NISC) ni wa kwanza kushuhudiwa na Kituo cha Uwekezaji (TIC) ambapo
utatoa kwa ajira za moja kwa moja 16,355 na ajira zilizokuwa za moja
kwa moja 200,000.
Akizungumza
wakati wa utiaji wa saini wa mikataba hiyo, Kijaji amezitaka taasisi
hizo kupunguza na kumaliza kabisa changamoto ya Tanzania kuagiza bidhaa
kutoka nje wakati uwezo wa kuzalisha hapa nchini upo.
Amebainisha
kuwa Serikali imekuwa ikiongeza nguvu kwa wakulima, ilikuweza kuzalisha
mali ghafi za kutosha zitakazoweza kuchakatwa na viwanda vya hapa hapa
nchini na kuzalisha bidhaa zitakazouzwa ndani na nje ya nchi.
Kijaji
amefafanua kuwa kama wanavyoenda kumaliza changamoto ya uagizaji wa
sukari mwaka 2024, amezitaka kampuni za uchakati wa mafuta kumaliza
kabisa kilio cha Watanzania kuhusu changamoto ya uhaba wa mafuta ya
kupikia ifikapo mwaka 2027 kwa kuzalisha mafuta tani 560,500 kutoka
tani 205,000 yanayozalishwa sasa.
"Haina haja ya kuagiza mafuta kutoka nje, wakati wapo wakulima ambao wanalima mbegu za kukamua mafuta.
Kilio
cha wawekezaji ilikuwa ni kuwepo kwa viwanda lakini wanakosa mali
ghafi, kwa sasa Serikali imewekeza huko tukafaye kazi" alisema.
Ameongeza
kuwa Serikali itazindua mtandao wa kituo kimoja kwaajili ya mwekezaji
kupata huduma zote sehemu moja, ili kumpunguzi usumbufu wa kutembea na
nyaraka katika kutafuta cheti.
Alisema
huduma hiyo itaweza kuwasaidia wageni wakiwa huko huko kuomba vibari na
kukamilika kwa siku tatu, ambapo haitakuwa na usumbufu kama ambao
ulikuwa zikijitokeza mwanzo kutokana utofauti wa kanuni na kisheria na
kufanya baadhi ya wawekezaji kushindwa kuwekeza.
"Nitaendelea
kuwaambia kwamba Tanzania sio kisiwa kama tupo peke yetu, mwekezaji
ukimsumbia anafanya kujadili na kwenda nchi zingine.
Kunasiku sio ghalama ni kuamua kwamba anahamisha, kwahiyo ni Jambo linalohitaji kuongea nao na sio kuwasumbua" alisema.
Katika
mikataba hiyo waliokuja kusaini katika makampuni 10, sita ni kutoka nje
ya Tanzania, watatu ni wawekezaji wa Tanzania ni mmoja anaubia wa
Tanzania na sekta binafsi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Gilead Teri amesema kuwa tangu
kuanzishwa kwa kituo hicho kwa mara ya kwanza ameshuhudia utiaji wa
saini wa mikataba ya utekelezaji na makampuni kumi kwa wakati mmoja.
Pia
amesema mikataba hii inaashiria mafanikio makubwa ya kihindi za
uboreshaji wa Mazingira ya Uwekezaji, kuongezeka kwa ufanisi wa utiaji
wa huduma kwa wawekezaji na kuimarika kwa juhudi za uhamasishaji
Uwekezaji hapa nchini.
"Tunashukuru
wawekezaji walioamua kuunganisha juhudi za Serikali kwa kuwaletea
wananchi maendeleo na kukuza uchumi kupitia Uwekezaji" alisema.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kuchakata Mafuta ya Wild Flower Gran's Oil, Azizi Omary
amesema wanatarajia kufikia kiwango hicho cha uchakataji wa mafuta kabla
ya muda waliopanga Serikali.
Aidha
amesema matarajio yao makubwa ni kuona kiwanda hicho kinatanuka zaidi
kutoka mkoani Singida kwenda Dodoma na mikoa mingine wanaozalisha mbegu
za mafuta.
"Tumejipanga na uwekezaji huu kuhakikisha, tunachakata mafuta ya kutosha" amesema
No comments:
Post a Comment