HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 30, 2023

Naibu Waziri Dkt. Kiruswa awaaga Wachimbaji, Wafanyabiasahra wa Madini, Watoa Huduma wanaokwnda China, awataka kutumia safari hiyo kujifunza

 Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameiaga Timu ya watu takribani 100 wakiwemo wachimbaji wadogo, wachimbaji wa Kati, Wafanyabiashara wa madini na watoa huduma migodini wanaotarajia kwenda nchini China.


Akizungumza jijini humo katika hafla ya kuuaga ujumbe huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Naibu Waziri Dkt. Kiruswa amewataka kuhakikisha safari hiyo inaleta tija kwa kuleta wawekezaji wengi na kupata vifaa vya kisasa ili kuongeza uzalishaji wa madini nchini.



Dkt. Kiruswa amesema kuwa, ubalozi wa China kwa kushirikiana na Kampuni ya Touchbroad ya nchi hiyo imeandaa ziara ya wachimbaji kutoka Tanzania ili  kuwawezesha kukutana na wawekezaji wa Sekta ya Madini nchini China, kutembelea viwanda vya kutengeneza mitambo na vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji wa madini na kuwawezesha kupata uzoefu na wafanyabishara wa madini waliopo China na kupata teknolojia za uchimbaji na uchenjuaji.


"Niwaombe kila mmoja wenu akiwa China ahakikishe anatimiza malengo yake kadri anavyoweza ili ujuzi mtakaoupata uje kuwasaidia kuboresha biashara zenu na kuongeza tija,” amesema Dkt. Kiruswa.


Vile vile, amezipongeza taasisi za fedha kwa kuendelea kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara katika kuhakikisha wanapata mikopo ya fedha kwa kuwa karibu na wafanyabiashara wa madini na amewataka kuangalia uwezekano wa kupunguza riba ili kupata wateja wengi na kuruhusu wachimbaji  wadogo kupata mikopo yenye riba ndogo.


Kwa upande mwingine, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amewataka wachimbaji hao kutumia ziara hiyo kujifunza na kupata uzoefu watakapotembelea  viwanda vya kutengeneza mitambo na vifaa vya uchimbaji.


Nae, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini nchini (FEMATA), John Bina amesema kuwa, ziara hiyo nchini China inakwenda kufungua milango ya nchi kuvutia wawekezaji wengi kuendelea kuja kwa kuwa nchi ina sera nzuri katika uwekezaji.


Viongozi wengine walioshiriki ni pamoja na  Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, Mbunge wa Viti Maalum Iringa Dkt. Rita Kabadi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. CPA Venance Mwasse, Mjumbe wa Bodi ya STAMICO Lucas Seleli, Mwakilishi wa Benki ya CRDB pamoja na wataalam kutoka Wizara na taasisi zake katika safari inayolenga kukutana na wawekezaji wa Sekta ya Madini nchini China.


Aidha wadau wengine, wanaoshiriki katika ziara hiyo ni wataalam wa madini kutoka taasisi za Wizara ya Madini, taasisi za Fedha ikiwemo Benki ya CRDB na wadau wengine muhimu.

No comments:

Post a Comment

Pages