Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (kushoto), akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja. Hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo Dar es Salaam jana chini ya kaulimbiu ya ‘Timu Yetu Nguvu Yetu.’ Matundu alisisitiza dhamira ya benki yake kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja ya Benki ya Exim Tanzania, Frank Matoro.
Na Mwandishi Wetu
Banki ya Exim Tanzania jana iliungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2023 inayoadhimishwa chini ya kaulimbiu ya ‘Team Service’ huku benki hiyo ikirejelea dhamira yake ya kuendelea kutoa huduma zinazokidhi matakwa ya wateja, ambayo ni moja ya msingi ya benki hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo iliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Mtundu alisema benki yake haichukulii huduma kwa wateja kirahisi ndiyo maana huduma ni miongozi mwa miiko na utamaduni wa benki yake.
Matundu alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya ‘Team Service’ inaendana hasa na falsafa ya Benki ya Exim na kuongeza kwamba huduma ni chachu ya biashara na benki hiyo imeweka kipaumbele cha huduma kwa wateja.
"Hii ndiyo sababu benki ya Exim inaendelea kuwekeza mara kwa mara katika teknolojia na kuwapa wafanyakazi wetu ujuzi na rasilimali zinazohitajika ilikuhakikisha wanawapa wateja wetu huduma za hali ya juu," Matundu alisema.
Alibainisha kuwa katika sekta yenye ushidani mkubwa kama vile benki ambapo taasisi nyigi zinaweza kutoa bidhaa na huduma zinazofanana, huduma kwa wateja na kuzingatia wateja ni mambo muhimu na hili limekuwa kipaumbele kwa benki yake kwa miaka mingi.
Matundu alisema benki yake imetoa kipaumbele kwa mteja-kwanza kama njia bora ya kutoa huduma ya kipekee hali ambayo inasaidia kuuza bidhaa na huduma za benki hiyo.
"Tumeweza kuishi ndani ya maadili yetu ya kubadilika, kutegemewa, uadilifu, taaluma, na kiu ya kuridhisha wateja wetu kila siku,kila siku ambayo imetufanya tuwe bora katika sekta ya benki ya Tanzania katika suala la huduma kwa wateja. Uongozi wetu unathamini kujitolea kwa wafanyakazi wetu na hii imekuwa muhimu katika ukuaji wa biashara yetu,” alibainisha.
Matundu alisema benki yake mwanzoni mwa mwaka huu aliboresha mfumo wake na kuweka miundombinu thabiti, hatua inayolenga kuimarisha utendaji wake na kuwapa wateja hali ya juu ya usalama, ufanisi na uvumbuzi.
"Hii inadhihirisha ari yetu katika kubadilika na kuwa zaidi ya taasisi ya benki. Kama benki, tumejitolea kuwekeza katika kuongeza uwezo li wa mifumo yetu ilikutoa huduma bora kwa wateja wetu na jamii inayotuzunguka. Lakini nina hakika kabisa kwamba faida ya ushindani katika benki itatokana na teknolojia inayoendeshwa na watu. Kama benki, hatuna chaguo ila kuendelea kuwapa wateja wetu thamani zaidi katika suala la utoaji huduma," alisema.
Kwa upande wa utendaji kazi, Matundu alibainisha kuwa benki ieendelea kufanya kazi kwa ufanis mkubwa kufuatia utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo kimamilifu ilikunufaisha wadau wote wa benki hiyo ikiwemo jamii kwa ujumla.
"Viashiria vyote yanaonyesha kuwa tunakua kama benki," alisisitiza.
Wakati wa hafla hiyo, aliipongeza idara ya huduma kwa wateja ya benki hiyo na wateja wake kwa kuendelea kuwa wafadhili na kujitolea kwa chapa ya Benki ya Exim, na kuwahakikishia kuwa benki hiyo itaendelea kukidhi na kuvuka matarajio yao kwa kutoa bidhaa na utoaji huduma bora.
“Uaminifu wa wafanyakazi wetu na wafanyakazi umeifanya Benki ya Exim kuwa mojawapo ya taasisi za fedha zinazopendelewa zaidi nchini kwa miaka mingi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja cha Benki ya Exim Frank Matoro wakati wa hafla hiyo alisema benki hiyo itaendelea kuwekeza kwa watu wake katika masuala ya ujuzi ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja wake.
"Kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu, huduma kwa wateja itaendelea kubaki msingi na hitaji la lazima kwa wafanyakazi wote wa Benki ya Exim na inapaswa kujumuisha idara zote ndani ya benki kwa kuwa tunafanya kazi kwa pamoja kama timu," Matoro alisema.
No comments:
Post a Comment