Na Victor Masangu, Kibaha
Katika
kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya
michezo mke wa Mbunge la Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ameanzisha
rasmi mashindano ya mchezo wa netiboli kwa wanawake wa Jumuiya ya Umoja Wanawake (UWT) Kata ya Misugusugu.
Mama Koka amezindua michuano hiyo ikiwa ni moja ya ahadi yake kubwa ambayo aliitoa ya kukuza na kuinua vipaji vya mchezo huo kwa wanawake wa kata zote 14 zilizopo katika Jimbo la Kibaha mjini ili kuweza kupata fursa ya wanawake kushiriki kikamilifu katika kukuza vipaji vyao.
Alibainisha
kwamba hivi karibuni aliweza kufanya ziara yake katika kata mbali mbali
akiwa Kama mlezi wa UWT Kibaha mji na alitoa na kukabidhi vifaa mbali
mbali kwa timu husika ikiwemo mipira pamoja na jezi lengo ikiwa ni kila
kata kuweza kuunda timu yao ya netiboli.
"Kwa
kweli nimefarijika sana leo kuwepo hapa katika kata ya Misugusugu ikiwa
nimekuja kuonana na wanawake wenzangu sambamba na kuzindua mashandano
haya ambayo tumeyapa jina la Selina Cup na mm lengo langu ni kukuza
vipaji zaidi katika mchezo huu wa netiboli,"alisema Mama Koka.
Kadhalika
aliwahimiza wanawake wote wa UWT kuwa na mshikamano katika kushiriki
katika mambo mbali mbali ikiwemo suala zima la michezo pamoja na
kukiimarisha chama Cha mapinduzi kuanzia ngazi za chini kabisa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji Elina Mgonja
alimpongeza Mke wa Mbunge kwa ushirikiano wake wa kujitolea na kuwa
karibu na jamii katika nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya michezo
hususan netiboli kwa wanawake.
Hivi
karibuni Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji alipokuwa katika ziara ya
Mwenyekiti wa UWT Kibaha mji aligawa vifaa mbali mbali vya mchezo wa
netiboli katika kata 14 kwa lengo la kukuza na kuinua na kukuza vipaji
vya wanawake wa Jimbo la Kibaha mjini.
No comments:
Post a Comment