Na John Marwa
Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya African Football League (AFL) Simba SC wamekaa kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara NBC PL baada ya kuwatungua Tanzania Prisons mabao 3-1 Dimba la Sokoine jijini Mbeya jioni ya leo.
Mnyama aliingia kwenye mchezo huo akihitaji ushindi licha ya kuuanza vibaya dakika ya 12 wakiruhusu bao kwa mkwaju wa free kick iliyowekwa wavuni na Edwin Balua.
Simba baada ya kuruhusu bao walirejea mchezoni kwa kuuchukua mchezo na kufanikiwa kuzawazisha kupitia mwamba wa Lusaka Clatous Chota Chama dakika ya 34 kisha dakika ya 45 John Bocco kupachika msumali wa pili.
Kipindi cha pili Saido Ntibanzokiza, alifungua akaunti ya mabao kwa kupachika bao la tatu na la ushindi kwa mkwaju wa penati baada ya Moses Phiri kuchezewa madhambi ndani ya boksi la Tanzania Prisons.
Kwa ushindi huo Simba wanakuwa wameshinda michezo minnne ya kwanza msimu huu sawa na asilimia 100 za ushindi, pointi 12, mabao ya kufunga 12 huku wakiruhusu mabao matatu. Klini shiti mbili.
Mchezo unaofuata kwa Mnyama Simba watasafiri hadi katikati mwa Tanzania kuwafuata Singida Big Stars siku ya jumapili katika Dimba la Liti mkoni humo.



No comments:
Post a Comment