*Zaeleza ziko tayari kushirikiana na Serikali, Wachimbaji*
*Dkt. Mwasse Azitoa Hofu Taasisi za Fedha
Na Mwandishi Wetu
Waziri
wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameichambua Vision 2030: Madini ni
Maisha na Utajiri na kuinadi kwa wadau mbalimbali wa Madini
zikiwemo Taasisi za Umma na binafsi zinazojishughulisha na Sekta ya
Fedha chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) kwa
kuonesha namna ilivyolenga kukuza uchumi na maisha ya Watu.
Amesema
Wizara imekutana na wadau hao ili kujadili mchango wa Sekta ya fedha
katika kuinua Sekta ya Madini na kueleza kuwa, sekta hiyo inao mchango
mkubwa wa kuiwezesha sekta ya madini kupiga hatua kupitia utoaji
mitaji na mikopo ikiwemo kutengeneza nafasi ya ushirikiano ili
kuimarisha zaidi Sekta ya Madini nchini.
Ameeleza
ikiwa kwa utafiti wa kina wa jiofizikia wa urushaji wa ndege ( high
resolution airborne Survey) umefanyika kwa asilimia 16 tu na Taasisi
ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) umeiwezesha sekta ya
madini kupiga hatua kubwa kiuchumi ikiwemo kuchangia asilimia 56 ya
thamani ya bidhaa za madini zilizouzwa nje katika Mwaka wa Fedha
2022/23, hivyo kufanyika kwa utafiti huo zaidi utaongezea tija zaidi.
Akifafanua
namna Sekta ya Madini inavyochangia kodi amesema imechangia kodi za
ndani kwa asilimia 15 ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni 2 pamoja na
kuchangia Dola za Marekani Bilioni 3.3. kutokana na mauzo ya bidhaa
zinazotokana na rasilimali madini kuongeza kuwa ikiwa wizara
itawezesha kufanyika kwa utafiti wa angalau kufikia asilimia 50 ifikiapo
mwaka 2030 kwa ushirikiano wa taasisi hizo, tafiti hizo zitaliwezesha
taifa kupiga hatua kubwa zaidi za kimaendeleo na kiuchumi kupitia
Sekta ya Madini.
‘’Tunataka
kufahamu taarifa za miamba, ili tupumike vizuri, hii ndiyo sababu ya
dira ya 2030. Ikifika 2030 tuwe tumefanya utafiti kwa nchi yetu kwa
angalau asilimia 50. Pamoja na mafanikio hayo bado machango wa sekta ya
madini haujakidhi matarajio ya watanzania na taifa letu, zipo
changamoto ndiyo sababu tumekutana kupitia kikao hiki kujadili
kuwaonesha kilichopo kwenye sekta ya madini, changamoto zilizopo na
kutuondoa tulipo,’’ amesema Mhe. Mavunde.
Akizungumzia
Madini ni Maisha na utajiri amesema haviwezi kutenganishwa maisha ya
mtanzania na Sekta ya Madini na kueleza kuwa kufanikiwa kwa tafiti za
kina na kupatikana kwa taarifa za awali, zitachochea sekta nyingine
kukua ikiwemo Sekta ya maji na kilimo na kueleza, ‘kilimo wana mkakati
wa kuchimba mabwawa 100, kupitia taarifa za GST inaweza kujulikana aina
ya maji na hivyo kufanya kilimo chake kwa tija na kuwezesha usalama
wa chakula na mapato.
Kuhusu
namna Sekta ya Madini inavyoweza kuokoa matumizi ya fedha za kigeni
kwa kununua mbolea kutoka nje, amesema zaidi ya tani 350,000 za
mbolea zinaagizwa nje kwa kutumia fedha za kigeni kwa ajili ya
matumizi ya kupandia, kukuzia na kustawisha , hivyo, taarifa za miamba
zitasaidia kujua miamba yenye malighafi zenye mbolea inayohiajika na
hivyo kusaidia shughuli za kilimo chenye tija.
‘’
GST imewahi kufanya utafiti wa kina mwaka 2004 kwa kurushwa ndege
katika maeneo ya Kahama, Biharamulo, Nachingwea na Mpanda kwa ukubwa
wa kilomita za mraba 30,000 tu ikilinganishwa na eneo la ukubwa wa
nchi ya Tanzania yenye ukubwa wa kilomita za mraba 945,000 ni kiasi
kidogo sana, ndiyo sababu tumekutana na ninyi tuwaeleze fursa ziizopo
kwenye Sekta ya Madini , tushirikiane,’’ amesema Waziri Mavunde.
Akizungumzia
madini mkakati ameeleza hivi sasa dunia imehamia kuzalisha nishati
safi isiyochafua mazingira ambapo madini yanayohitajika kuzalisha
nishati hiyo ni pamoja na madini ya graphite, colbat, manganese, nikeli
na kueleza kuwa, Tanzania inayo nafasi kubwa ya kuwa mzalishaji wa
madini hayo kwa kuwa yanapatikana nchini na kuongeza , ifikapo mwaka
2050 mahitaji ya madini hayo duniani yatafikia tani milioni 150.
Kufuatia
hali hiyo, amesema Sekta ya Madini ni sekta ambayo endapo
itafungamanishwa na sekta nyingine itawezesha watu kupata mafanikio,
tija, uwekezaji na maendeleo na kueleza kuwa Serikali imedhamiria
kutekeleza azma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwekeza kwenye
utafiti wa madini mkakati.
Kwa
upande wake, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt.
Venance Mwasse wakati akitoa wasilisho amesisitiza kuwa uchimbaji
mdogo ni eneo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa jicho la pekee na taasisi
za fedha na kueleza kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi
Kisheria katika shughuli za uchimbaji mdogo ikiwemo kuliwezesha
Shirikisho la Vyama Vya Wachimbaji Tanzania (FEMATA) kuwa na uwakilishi
Tume ya Madini, kuwatengea maeneo na kuwapatia elimu.
Amezieleza
changamoto za ukosefu wa masoko, teknolojia duni, kutokukopesheka,
elimu, na kueleza kuwa, tayari STAMICO imechukua hatua kadhaa ikiwemo
kuandaa mpango kutoa elimu kwa kuzunguka nchi nzima, kusaini
makubaliano na GST kuwezesha kupatikana kwa taarifa za kijilojia,
kusaini hati za makubaliano na baadhi za benki ikiwemo CRDB, KCB na NMB
na kuelezakuwa, hayo yote yamefanyika ili kupunguza hatari kwa
taasisi za fedha na hivyo kuzitaka taasisi hizo kujenga imani na
wachimbaji kwa kuwa tayari Serikali imeingilia kati ikiwemo
kuwarasimisha.
Ametolea
mfano wa ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa
Australia, Down Under na kueleza namna nchi ya Tanzania ilivyokuwa
kivutio katika mkutao huo kwenye madini mkakati na kueleza kuwa,
taasisi za fedha zinapaswa kutumia fursa za mazingira ya ndani
kuwawezesha wachimbaji wadogo kuweza kuchimba madini hayo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa TBA Theobas Sabi amesema anaishukuru
Wizara kwa mkutano huo ambao umeziwezesha tasisi za fedha kuielewa
Sekta ya Madini, pia amesema kutokuwepo kwa taarifa za kujua kiasi cha
madini kilicho kwenye leseni za wachimbaji ni eneo ambalo limekuwa
changamoto kwa mabenki na kueleza kuwa, taasisi hizo zitayachukua
yaliyozungumzwa katika mkutano huo kwa ajili ya kuyajadili kwenye vikao
kazi vya jumuiya hiyo.
Mbali
na taasisi za fedha, wengine waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na
wafanyabiashara wa madini, watoa huduma, wahimbaji Wadogo, Wa kati
Wakubwa. Aidha, wadau hao wamepongeza kwa hatua ya wizara kuitisha
kikao hicho.


No comments:
Post a Comment