January 05, 2013

BENITEZ ATAMBIA USAJILI WA DEMBA BA STAMFORD BRIDGE


LONDON, England

KOCHA Rafael Benitez amesisitiza kuwa usajili wa mshambuliaji Demba Ba sio kamari kwa klabu yake ya Chelsea na kwamba hakuna mtu mwenye furaha juu ya ujio Msenegal huyo kama Fernando Torres.

Torres alikuwa na msimu mbaya uliopita, wakati aliposhindwa kuchomoza kikosini mara kwa mara mbele ya mpachika mabao mahiri Didier Drogba aliyeihama klabu hiyo kiangazi kilichopita na kujiunga na Shanghai Shenhua.

Lakini Benitez kocha wa muda wa Blues kuelekea mwisho wa msimu huu, amesema mambo ni tofauti kwa sasa, ambapo Torres anakaaribisha ushindani katika nafasi yake dimbani.

Ba, 27, alimaliza usajili ulioigharimu Chelsea kitita cha pauni milioni 7.5 akitokea Newcastle United, ambapo leo anatarajiwa kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha matajiri hao wa jiijini hapa, katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Southampton.

Na Benitez amekubali kuwa Torres atapata wasaa wa kumpumzika katika baadhi ya mechi, kutokana na kucheza mfululizo msimu huu, ambao ameshuka dimbani mara 31 katika kikosi cha kwanza.

Benitez alisema: “Fernando ana furaha kuona klabu inasajili wachezaji wazuri, kwa sababu hiyo inamaanisha kwamba watashinda mechi nyingi zaidi wakiwa pamoja.

“Nilifanya naye mazungumzo wiki chache zilizopita na alisema kama klabu tunahitaji nyota zaidi. Sote tunatambua kuwa yeye amecheza mechi nyingi zaidi msimu huu na hutukuweza kuwa na chaguzi nyingi zaidi katika baadhi ya maeneo katika kikosi chetu, hasa katika ushambuliaji.

“Kwa kuondoka kwa Daniel Sturridge klabu Stamford Bridge, hiyo inamfanya Fernando kuwa mshambuliaji mkuu wa kati ambalo kimsingi nalo ni tatizo,” alisema Benitez.

No comments:

Post a Comment

Pages