Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

.

CRDB

CRDB
.

Pages

SERIKALI YAZUIA SH. BILIONI 5.5 ZA UJENZI WA MRADI WA SOKO LA KISASA LA MAGOMENI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akisikiliza maelezo ya Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Justin Lukaza, kuhusu ramani ya Mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam lenye ghorofa tatu ambalo limepewa kiasi cha Sh. bilioni 3.5, huku utekelezaji wa mradi huo ukiwa unasuasua. (Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)
 Muonekano wa eneo la Mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam, ukiwa katika hatua za awali za maandalizi, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipotembelea mradi huo ambao hadi kukamilika kwake utagharimu Sh. bilioni 9. 

 Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Serikali imezuia Sh. bilioni 5.5 ambazo zilipaswa kutumika kutekeleza mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni, liliko wilaya ya Kinondoni,  Jijini Dar es Salaam kutokana na kucheleweshwa kwa utekelezaji wa mradi huo licha ya kupewa fedha za kutosha kwa awamu ya kwanza.
Hatua hiyo imechukuliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi huo unaotarajia kugharimu shilingi bilioni 9 na kukuta ujenzi wake unasuasua.
Dkt Kijaji alisema kuwa  Serikali, imeipatia Manispaa ya Kinondoni shilingi bilioni 3.5 tangu mwezi Mei, 2018 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ambao ungepaswa ukamilike ndani ya miezi tisa tangu kusainiwa kwa mkataba wa ruzuku hiyo lakini ameshangaa kutomkuta mkandarasi kwenye eneo la ujenzi.
“Serikali inasitisha kutoa kiasi cha Sh. bilioni 5.5 mpaka watakapo dhihirisha wako tayari kuwahudumia wananchi na kutekeleza dhamira njema ya Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya kuwahudumia wananchi wake”, alieleza Dkt. Kijaji.
"Jana Manispaa ya Ilala wametuangusha kwenye usimamizi wa mradi wa Machinjio ya kisasa ya Vingunguti tumerejesha shilingi bilioni 3 Hazina na leo Manispaa ya Kinondoni nao wametuangusha na tunalazimika kuzizuia fedha hizo sh. bilioni 5.5 mpaka tujiridhishe na maendeleo ya ujenzi" alisisitiza Dkt. Kijaji
Awali, akitoa maelezo ya mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi wa Manispaa hiyo Justin Lukaza, ameeleza kuwa Manispaa hiyo imeingia mkataba wa kujenga soko hilo litakalo kuwa na ghorofa tatu na Kampuni ya Group Six International na kwamba ujenzi ungekamilika katika kipindi cha miezi sita ijayo na kutofautiana maelezo na mwakilishi wa Mkandarasi ambaye alimweleza Dkt. Kijaji kuwa ujenzi huo ungechukua muda wa  miezi 12.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Daniel Chongolo, amekiri kuwa kuna uzembe umefanywa na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni uliosababisha mradi huo kuchelewa kuanza na kumwomba Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ampe muda mfupi wa kurekebisha kasoro hizo.
Alisema kuwa tayari kuna hatua mbalimbali zilichukuliwa kwa maafisa waliofanya uzembe katika utekelezaji wa mradi hapo awali na hakujua kama bado kulikuwa na uzembe uliokuwa unaendelea baada ya kuchukua hatua hizo kwa sababu aliamini watendaji waliokabidhiwa kusimamia ujenzi wa mradi huo walijifunza kutokana na makosa ya wenzao walioondolewa kusimamia mradi huo
"Mimi nakubaliana na wewe (Naibu Waziri wa Fedha) kwamba kuna uzembe na kazi yetu sisi ni kuhakikisha tunarekebisha haya makosa na nichukue dhamana na tutawajika na watu hawa na nitalazimika kutumia dhana ya punda mwenye mzigo na mwenye punda anaye mchapa bakora ili punda aende" alisisitiza Bw. Chongolo
Baadhi ya wakazi wa Kinondoni, wameipongeza Serikali kwa ufuatiliaji wa miradi ya wananchi na kusikiliza kero zao wakitolea mfano wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, na kwamba hatua hiyo inaleta uwajibikaji wa watendaji ambao walijenga mazoea ya kuzembea kwa makusudi kusimamia miradi ya wananchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuliletea Taifa maendeleo
Mradi wa Soko la Kisasa la Magomeni ni miongoni mwa miradi 22 iliyopewa ruzuku na Serikali katika Mpango wa Awamu ya Kwanza wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato ambapo zaidi ya shilingi bilioni 147 zilitolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA TIC AIPA MWEZI MMOJA KUUNGANISHA MFUMO WA KIELEKTRONIKI UCHATAJI WA MIRADI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akipata ufafanuzi kuhusu huduma za mahala pamoja kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wawekezaji Bi Anna Lyimo, Waziri Kairuki alifanya ziara kwenye ofizi za TIC leo February 20, 2019.
 Mkurugenzi Mtendahi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Geoffrey Mwambe akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angela Kairuki alipotembelea kwenye ofisi hizo leo February 20, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akitoa ufafanuzi wa jambo alipotembelea kwenye ofisi za kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Mapema February 20, 2019 ili kujionea baadhi ya kazi zinazofanywa na kituo hicho sehemu ya huduma za mahala pamoja
 
Na Grace Semfuko-MAELEZO
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji ) Angela Kairuki amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kupitia mfumo wa huduma za mfumo wa mahala pamoja kuboresha utoaji wa huduma kwa wawekezaji kupitia mfumo wa kielektroniki na kuwaagiza kuunganisha mfumo wa dirisha la uchakataji miradi (TIW) kwenye Kanda zote saba za kituo hicho Nchini ili kurahisisha mwenendo wa upatikanaji wa huduma  kwa wawekezaji.

Kairuki alisema mfumo huo unasaidia kuondokana na urasimu,ucheleweshwaji na unarahisisha upatikanaji wa leseni,cheti na  vibali ambao utasaidia kuongeza wawekezaji nchini ambapo kati ya kanda saba za TIC ni kanda moja tu ya Kaskazini ndio iliyoingizwa kwenye mfumo na kuagizwa kanda zingine ziharakishe mfumo huo ndani ya mwezi mmoja.

Waziri Kairuki aliyasema hayo February 20, 2019, baada ya kuzungumza na maafisa wanaotoa huduma ndani ya mfumo wa mahala pamoja na kufanya nao majadiliano juu ya namna ya kuboresha huduma hizo ambazo zinatolewa na taasisi 11 ndani ya jengo la TIC.

 “Mfumo wa huduma za mahala pamoja ni mzuri sana, lakini tuhahitaji kuyafanyia kazi masuala kadhaa kwenye kila taasisi 11 zilizopo kwenye huduma za mahala pamoja ili kuondokana na changamoto ambazo zinachelewesha upatikanaji wa huduma za uwekezaji” alisema Kairuki.
Aidha aliwataka watendaji wa ardhi ndani ya kituo hicho kuweka vizuri takwimu za ardhi ya uwekezaji na kushughulikia changamoto za upatikanaji wa ardhi kwa wawekezaji ambao unasimamiwa na TIC.

Akiwa katika sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Waziri Kairuki aliagiza  watendaji hao kuuona umuhimu wa utoaji  wa  cheti cha utambulisho wa namba ya mlipakodi  TIN kwenye Kituo hicho ili kurahisisha huduma kwa wawekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkurugenzi  wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe alisema iwapo Serikali itawezesha taasisi zote zinazohusika na huduma za mahala pamoja kutoa huduma zake stahiki zinazohusu uwekezaji ndani ya ofisi za TIC itakuwa ni hatua kubwa katika uwekezaji.

“Taasisi zilizopo ndani ya mfumo wa mahala pamoja zinafanya kazi kubwa, tunachoomba sisi kama TIC ni kwamba huduma za taasisi hizo kwa wawekezaji zikamilike ndani ya TIC badala ya kwenda kwenye makao makuu ya ofisi hizo kufuata idhini ya vibali,leseni na vyeti husika kwa wawekezaji” alisema Mwambe.

Nae Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wawekezaji Anna Lyimo alisema kwa sasa huduma za mahala pamoja zimekuwa na manufaa makubwa kwa wawekezaji kutokana na kuwapo kwa taasisi zote muhimu Kituoni na kwamba marekebisho yaliyotajwa na Waziri yatafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo.

“Tumeyapokea maagizo ya Waziri na tutayafanyia kazi, ni maagizo yenye tija kwa kituo” alisema Kaimu Mkurugenzi Idara ya  Huduma za Mahala Pamaoja wa  TIC Anna Lyimo.
Huduma za mahala pamoja kwenye kituo cha uwekezaji Tanzania TIC zinajumuisha taasisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Baraza la Taifa la usimamizi na uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Shirika la viwango Tanzania (TBS), Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Wizara ya Ardhi, Idara ya Uhamiaji, Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA),

DC NA DED BIHARAMULO JIREKEBISHENI-MAJALIWA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wende Ng’ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais Dkt. John Magufuli kufanya maamuzi mengine.

Amesema kitendo cha viongozi hao kutoelewana kinaonesha mfano mbaya kwa watumishi walio chini yao, hivyo amewataka wajirekebishe mara moja kwani wameaminiwa na Serikali kuliongoza eneo hilo na si kuwachanganya wananchi.

Waziri Mkuu ametoa kalipio hilo leo (Jumatano, Februari 20, 2019) wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi, kijiji cha Nyakanazi, Biharamuko mkoani Kagera.

Amesema kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika wilaya. “Mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana.”

Awali, Waziri Waziri Mkuu akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera alitembelea kambi ya Nyanza Roads inayojenga barabara ya Nyakanazi-Kabingo, inayounganisha mikoa ya Kigoma na Kagera na kusema kuwa hajaridhishwa na kasi ya mkandarasi huyo.

Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami inaurefu wa kilomita 50 na ilianza kujengwa 2014 ilitarajiwa kukamilika 2016, ambapo kwa sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 60.

“Sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hii, mkandarasi na mhandisi mshauri wote wanaonekana hawapo makini katika kufanya kazi hii. Hii ni aibu kwa wakandarasi wa ndani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia kutokupewa kazi kumbe hawako makini.”

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 20, 2019.

MHE KANYASU AOMBA UMEME WA REA GEITA MJINI

Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameomba umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA katika jimbo la  Geita mjini kutokana na sababu kuwa  Geita mjini, mjini ni kata mbili tu ikiwemo Kalangalala, Bombambili na maeneo yote yaliyobaki ni vijiji.
Pia, Mhe.Kanyasu amemuomba Waziri wa Nishati, Dkt.Medald Kalemani kuharakisha zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo ya  yaliyoyopitiwa na umeme huo kwa vile tokea mradi huo ulipozinduliwa mwaka jana, kijiji kimoja  tu katika jimbo hilo ndo kimenufaika na mradi huo.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge huyo wakati wa uzinduzi wa umeme wa REA uliofanyika katika kijiji cha ibanda katika wilaya ya Geita mkoani Geita, eneo ambalo  linalohesabika kuwa ni mtaa.
Akizungumza kabla ya kuzindua umeme huo, Dkt.Meldard Kalemani ametaja sababu zilizoifanya Geita mjini kuchelewa kupata umeme wa REA kwa vile Geita mjini inahesabika kuwa ni  mjini na mjini hakuna  vijiji bali kuna mitaa.
"Sisi tuliambiwa tupeleke umeme kwenye vijiji na sio kwenye mitaa, Mhe. Kanyasu ndo kapigania kutuambia kuwa hii sio mitaa bali ni vijiji" Amesisitiza Waziri Kalemani
Hata hivyo, Waziri Kalemani amemhakikishia Mbunge wa Geita mjini kuwa jumla ya vijiji 42 tayari vipo kwenye mpango wa kuunganishwa na mradi wa umeme wa REA.
Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani amewaagiza  Wakandarasi na Wataalamu wote kuwa hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba wahakikishe kila mhitaji anaunganishiwa umeme haraka iwezekanavyo.
Aidha, Waziri Kalemani amepiga marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme zaidi ya shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa mwananchi atayetozwa zaidi ya kiasi hicho atoe taarifa ili hatua kali dhidi ya wahusika ziweze kuchukiwa.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa kwa gharama hizo kwani baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu za Shirilka la Ugavi wa umeme Tanzania(TANESCO

WAMILIKI VIWANDA VYA KUCHAKATA MAGOGO WARUHUSIWA KUTUMIA MASHINE ZA ZAMANI

Meneja wa Shamba la Miti la North Kilimanjaro (Rongai)  Ernest Madata (Katikati) akimuongoza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu (kushoto)  alipotembelea vitalu vya miti katika shmaba hilo .kulia ni Afisa Misitu Emanuel Kiyengi.
Meneja wa Shamba la Miti la North Kilimanjaro (Rongai)  Ernest Madata akiumuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu sehemu ambayo huoteshwa mbegu za miti mbalimbali.
Meneja wa Shamba la Miti la North Kilimanjaro (Rongai)  Ernest Madata akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu sehemu ya vitalu vya miti vinavyoandaliwa na shamba hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu akitizama kitalu cha miti iliyo tayari kupelekwa shamba kwa ajili ya kuoteshwa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu akitizama mche wa mti uliooteshwa katika kitalu cha Shamba la Miti la North Kilimanjaro.
Sehemu ya vitalu vya miti katika shamba la miti la North Kilimanjaro .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu akiotesha mche wa mti katika eneo la vitalu vya kuandaa miche ya miti katika shamba la miti la North Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu akimwagia maji mche wa mti aliuotesha katika eneo la vitalu vya kuandaa miche ya miti katika shamba la miti la North Kilimanjaro.
Meneja wa Shamba la Miti la North Kilimanjaro (Rongai)  Ernest Madata akumueleza jambo Naibu Waziri ,Kanyasu alipofika eneo ambalo shughuli ya uvunaji wa miti inafanyika.
Sehemu ya Msitu uliopo kwenye shamba la miti la North Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu akizungumza na watumishi wa Mashamba ya Miti ya North Kilimanjaro na West Kilimanjaro alipofanya ziara ya siku moja ya kutembelea mashamba hayo.
Baadhi ya watumishi wa Mashamba ya West Kilimanjaro na North Kilimanjaro wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu .
Meneja wa Shamba la Miti la North Kilimanjaro ,Ernest Madata akizungumza katka kikao hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini


SERIKALI imeruhusu Wamiliki wa viwanda vya kuchakata Magogo kwa ajili ya kutengeneza Mbao kuendelea kutumia Mashine za zamani wakati wakiwa katika mchakato wa kujielekeza kwenye mabadiliko ya teknolojia .

Hatua ya serikali inatokana na ombi la Wadau wa misitu walilotoa wakati wa ziara ya siku Moja ya Naibu Waziri wa Malisili na Utalii ,Constantine Kanyasu alipotembelea Mashamba ya Miti ya North Kilimanjaro maarufu kama Rongai na West Kilimanjaro.

Mh Kanyasu pia akazungumzia suala la mgao mdogo wa Magogo kwa wachakataji huku akiahidi kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuona namna ambavyo wadau hao watasaidika. 

Meneja wa Shamba la Miti la North Kilimanjaro ,Ersnest Madata amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni mahitaji makubwa ya mazao ya misitu katika viwanda ukilinganisha na uwezo wa Shamba hilo.

Mapema katika kikao cha Wadau wa Misitu na wafanyakazi wa mashamba ya miti ya West Kilimanjaro na North Kilimanjaro wamiliki wa viwanda vya kuchakata mazao ya misitu na wanunuzi wa mazao hayo wakapata nafasi ya kutoa kero zao kwa naibu Waziri Kanyasu.

Mashamba ya Miti ya North Kilimanjaro na West Kilimanjaro yanaukubwa Heksri 15701 yakiwa yamepakana na nchi ya Kenya ,Wilaya ya Longido mkoani Arusha na Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.

WATEJA WA HALOTEL KUPIGA SIMU, KUTUMIA INTANETI BILA KIKOMO

 Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung, akizunguka wakati wa uzinduzi wa huduma mpya za Royal Bundle na Tomato Bundle uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Feb, 19, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung, akizungumza katika hafla hiyo.
 Wageni waalikwa, wasanii mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Halotel wakiwa katika hafla hiyo.

Mkuu wa Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya za Royal Bundle na Tomato Bundle uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Feb, 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Halotel, Do Le Hoan na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung.

Mkuu wa Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya za Royal Bundle na Tomato Bundle uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Feb, 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Halotel, Do Le Hoan na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung.

Wafanyakzi wa Halotel pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.

Baadhi ya wasanii na watangazaji waliohudhuria hafla hiyo.

Baadhi ya maofisa wa Halotel wakiwa katika uzinduzi huo.

Kabla ya uzinduzi.

Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung, akiteta jambo na Ofisa Uhusiano wa Halotel, Stellah Pius.

Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung akijadiliana jambo na Mkuu wa Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda.

Mkuu wa Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa Halotel, Stellah Pius.
 Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung,akisalimiana na msanii wa Bongo Fleva, Mr. Blue.
 Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung,akijaribu kufungua Champagne.
Mhina Semwenda akifungua Champagne.
Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung (wa pili kushoto). akigonga tano na Mkuu wa Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda pamja na wasanii waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa huduma mpya za Royal Bundle na Tomato Bundle.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Halotel imeanzisha huduma mbili mpya zijulikanazo kama Royal Bundle na Tomato Bundle, zote zikilenga kumrahihishia mteja katika huduma za kupiga simu pamoja na intaneti kwa gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Jijini Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Truang alisema huduma hizo pia zimelenga kuongeza ubora katika utoaji wa huduma za simu kupitia mtandao huo hapa nchini.

Alisema huduma ya Royal Bundle, imeanzishwa kama moja ya ubunifu wa kukata kiu ya wateja ambao walikuwa wanatamani kutumia huduma bila kupata shida ya aina yoyote ikiwemo ya kuisha muda wa maongezi au intenet kukata wakati wakiendelea kuongea au kuperuzi.

“Tunatambau umuhimu wa sekta ya mawasiliano katika shuhuli za kiuchumi hivyo tusingependa kampuni yetu kikwazo katika kulifanikisha hilo na ndiyo maana leo tunawatangazia huduma wa huduma hizo nchini” alisemaTruang.

Aliongeza kuwa kupitia huduma hiyo kwa sasa watumiaji wa mtandao wa Halotel kwa kiasi cha Sh 10,000 wanaweza kupiga simu za ndani na za kimataifa kwa nchi za Marekani, China,Canada,India na zinginezo sambamba na kutuma sms bila kikomo .

Alisema faida zingine kwa mtumiaji wa mtandao huo ni pamoja na kujipatia muda wa maongezi wa dakika 520 kwa Sh 10,000 atakayokuwa ameiongeza katika simu yake ambazo zitamuwezesha kupiga simu kwenda mitandao yote pamoja na kuwezeshwa kifurushi cha inteneti cha GB 2.

Aidha kuhusu kifurushi cha Tomato Bundle, Naibu Mkurugenzi huo alisema kupitia huduma hiyo, mteja na watumiaji wa Halotel nchi nzima wataweza kupiga simu halotel kwenda halotel kwa dakika tano bure za mwanzo katika kila simu atakayopiga pamoja na kupata salio la Sh 4000 ambalo atalitumia kwenye huduma nyingine za Halotel kwa kipindi cha mwezi mzima.

SERIKALI YAPANIA KUINUA ZAO LA PARACHICHI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

Na Josephine Majura na Ramadhani Kissimba, WFM-Mbeya


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na Wakulima na Wawekezaji wa zao la parachichi katika Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya. Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki uliwakutanisha wataalam kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na wadau wote wa zao la Parachichi.

Waziri Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda unaoendana na maendeleo ya Sekta ya Kilimo na katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Mkakati wa Pili wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Serikali imeweka msukumo mkubwa kwenye mazao yenye thamani kubwa ikiwepo zao la parachichi.

Amesema nafasi ya sekta ya kilimo ni kubwa katika kujenga uchumi wa nchi, kutokana na ukweli kwamba theluthi mbili ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo, hivyo kuinua kilimo cha parachichi kitasaidia kuongeza ajira na kipato kwa vijana.

‘Parachichi ni zao jipya lakini lina thamani kubwa sana, ulimwenguni linajulikana kama dhahabu ya kijani’ alisema Dkt. Mpango.

Amewataka wakulima wa zao hilo kuhakikisha Tanzania inakuwa kinara wa uuzaji wa parachichi nje ya nchi ili kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla.

"Ili kuzalisha kwa wingi zao hili Wakulima wetu hasa wadogo wadogo wanatakiwa wawe na mitaji, utaalamu, sehemu ya kuhifadhia mazao yao na kuwepo na masoko ya kuuzia zao hilo, hasa masoko ya nje ambayo yataingizia nchi fedha za kigeni" aliongeza Dkt. Mpango

Mhe. Mpango amesema Serikali itaendeleza sekta ya kilimo kwa kuwa ndio sekta mama katika Taifa, inayozalisha malighafi za viwandani na kuliingizia fedha nyingi za kigeni.


Awali akimkaribisha Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amesema Mkoa wa Mbeya ni ukanda maalum katika mazao ya Kilimo, ukiacha zao la Parachichi ambalo linazalishwa kwa wingi Wilayani Rungwe, pia Wilaya hiyo ni maarufu kwa kilimo cha ndizi na viazi, mazao ambayo yanatoa fursa kubwa kwa kutoa ajira kwa wananchi wa Mbeya na kukuza uchumi wa Taifa.

Kikao hicho cha wawekezaji na wakulima wa zao la Parachichi mkoani Mbeya, kimehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe.

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MWEKA HAZINA KIBONDO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati  alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo,  Februari 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya  ya Kibondo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Februari 19, 2019.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya  ya Kibondo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Februari 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Februari 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga.

KIBONDO, KIGOMA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Thomas Chogolo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma  zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo.

Pia, Waziri Mkuu amewataka watendaji wa halmashauri huyo kumaliza haraka migogoro yao ya kiutendaji kabla ya Serikali haijawachukulia hatua kwani wanachokifanya ni kinyume na maelekezo yake.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo leo (Jumanne, Februari 19, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma.

“Katika Serikali hii suala la ukusanyaji wa mapato ni jambo nyeti na limepewa kipaumbele, hivyo ni lazima fedha inayokusanywa itumike kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.”

Waziri Mkuu amesema wananchi wa halmashauri hiyo wanalipa kodi kupitia kwa watendaji wa kata katika maeneo yao lakini  Mweka Hazina haingizi kwenye mfumo wa Serikali. “Jambo hili halivumiliki.”

Amesema mbali na fedha za makusanyo ya kodi pia matumizi ya fedha mbalimbali zinazopelekwa na Serikali katika halmashauri hiyo nayo hayaridhizishi. Ametoa mfano wa fedha za sekta ya Afya ambapo zaidi ya bilioni mbili zimepelekwa na dawa hakuna.

Waziri Mkuu amesema uaminifu na uadilifu ni jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na watumishi wa umma, hivyo amewataka watumishi hao wasijiingize kwenye mambo ambayo hayana tija katika utumishi wao.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imewapa dhamana watumishi hao kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si kutanguliza maslahi yao binafsi, amewataka wajirekebishe kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Serikali haitawapa nafasi ya kuendeleza migogoro yenu kila mmoja lazima atambue majukumu yake na kuyatekeleza. Serikali haiitaji mtumishi mvivu, masiyekuwa muadilifu na wala anayejihusisha na vitendo vya rushwa.”

Amesema ni lazima wakamaliza migogoro ya kiutendaji ambayo imesababisha watendaji wa halmashauri kutoelewana na kugawanyika katika makundi na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 19, 2019.