January 12, 2013

BREAKING NEWS, AJALI MBAYA YATOKEA POSTA JIJINI DAR ES SALAAM

 Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakimshusha mwenzao baada ya kujigonga kwenye mti na kujeruhiwa vibaya na kupasuka sehemu za kichwani wakati akiwa kwenye Lori lenye namba za usajili 5514 JW 07 aina ya IVECO kandokando ya barabara ya Samora jirani na Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam jioni hii. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Baadhi ya wasamalia wema wakimpeleka hospitali majeruhi huyo.
 Majeruhi akiingizwa katika Bajaji tayari kwa ajili ya kupelekwa hospitali.
 Lori aina ya IVECO ambalo majeruhi huyo alikuwa amepanda huku likiwa limesheheni mzigo mkubwa.
 Hii ndio Barabara ya Samora ilipotokea ajali hiyo. 
Hapa ndipo alipojigonga majeruhi na kupasuka sehemu za kichwani.

No comments:

Post a Comment

Pages