January 27, 2013

Izzo Business kutoka na ‘Ball Player’


Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa Hip hop nchini, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Business’ anajipanga kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ball Player’ ambayo amewashirikisha wakali wa muziki huo, Quick Rocka na Albart Mangwea ‘Ngwea’.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Izzo Business alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho ambapo anatarajia kukisambaza mwisho wa wiki hii.

“Naimani kazi hii itafanya vizuri katika soko la muziki huu kwani mashairi yake yamesimama na yanaujumbe mzito katika jamii naomba mashabiki wa muziki huu wakae mkao wa kula,” alisema Izzo Business.

Alisema kazi hiyo kaitengeneza kwa mtayarishaji maarufu hapa nchini ambaye anafanya vizuri, Lamar na kwamba kwasasa anajipanga kutengeneza video ya kazi hiyo.

Msanii huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Ridhiwan’ mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo alivifanya na kulishika soko la muziki huo.

No comments:

Post a Comment

Pages