HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 25, 2013

MAULID YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) VIWANJA VYA MAISARA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Viongozi wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana, na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,(katikati).
 Ustadh Abdulla Hamad wa Chuo cha Kiislamu,akitoa tafsiri ya Aya za Quran,zilizosomwa na Ustadh Rashid Jaffer wa

Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu. 

 Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu. [Picha na Ramadhan

Othman,Ikulu.]

 Wake za Viongozi na Akinamama wakisikiliza Maulid Barzanj ya Kuzaliwa kwa yaliyosomwa na wasomaji mbali mbali na Qasida katika  sherehe za Maulid  ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar. 
 Ustadh Ali Twalib Mohamed,wa Kibanda Hatari Mjini Zanzibar akisoma Maulid Barzanj Mlango wa kwanza katika kusherehekea kwa kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
 Wanafunzi wa Madrasa  Munawara Shaurimoyo  Wilaya ya Mjini Zanzibar wakisoma Qaswida  ya Mwaka 1434 el Hijra,wakati wa sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisra Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria katika sherehe za Maulid  ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis,iliyotayarishwa na jumuiya hiyo  katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipeana mkono wa Shukurani na
Sheikh Sherali Champsi,Mwenyekiti wa Maandalizi  wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar,baada ya kupeka zawadi aliyokabidhiwa na  Sheikh Khamis Haji Khamis,(katikati) iliyotayarishwa na jumuiya hiyo  katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia ubani kama ishara ya ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya
Kiislamu. 

No comments:

Post a Comment

Pages