January 27, 2013

MTIKILA AMTAKA KIKWETE KUTUMIA HEKIMA MGOGORO WA GESI


DAR ES SALAA, Tanzania
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Christopher Mtikila, amemtaka Rais Kikwete kutumia hekima katika kumaliza mgogoro wa gesi na maslahi ya Mtwara kinyume chake nchi inaweza kugawanyika.

Akizungumza na wandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mtikila alisema kuwa madai ya kwamba umeme wa gesi hiyo ufuliwe kulekule Kusini yanatokana na uchungu wa wananchi wote wa Kusini.

Alisema iwapo moto wa mgogoro huo hatauzimwa kwa hekima si ajabu ukaimeza mikoa yote ya Kusini ikiwemo Lindi, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Morogoro na hata Rukwa  ambapo matokeo yake kuzaliwa mataifa mawili mpaka ukiwa reli ya kati.

Mtikila alisema wakazi wa kusini hawazuii gesi hiyo isitoke bali wanachotaka umeme huo ufuliwe kule kule, lengo likiwa ni kuwaletea mapinduzi ya maendeleo.

“Wananchi wa Mtwara wanafahamu kwamba sumaku ya mandeleo ya uwekezaji wa miradi mikubwa ya kuwaletea maendeleo ni nishati na miundombinu, lakini watawala wa CCM waliwanyang’anya reli ya kusini kwa uharamia wa kung’oa mpaka mataruma na kufutilia mbali hata na tuta lenyewe,”alisema.

Aliongeza kuwa Rais Kikwete analazimika pia kutamka bayana kipaumbele kwa uboreshaji wa Bandari Kuu ya Mwara, ikibidi hata kwa kusitisha mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Kwamba njia pkee ya kuzima moto huo kusini na kurejesha amani  ni Rais huyo kutoa tamko la kukubali kufuliwa umeme huo mkoani Mtwara kwa ajili ya maslahi ya Taifa.
  

No comments:

Post a Comment

Pages