January 12, 2013

MWAKA 2013 NI WA MABADILIKO KATIKA TASNIA YA SANAA-STEVEN NYERERE


Na Elizabeth John

“Sanaa inalipa sana lakini wasanii wenyewe hatupo makini na kile tunachokifanya ndio maan ahatupigi hatua, nchi kama Kenya au Nigeria wasanii wanafaidika na kazi zao kwasababu wapo makini na wanajua wanachokifanya,” 

MSANII  wa vichekesho nchini, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ amesema mwaka 2013 amepania kuleta mabadiliko katika tasnia ya sanaa hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Steve Nyerere alisema Tanzania tupo nyuma sana katika sanaa kuliko nchi nyingine hivyo yeye amejipanga kuleta mabadiliko.

“Sanaa inalipa sana lakini wasanii wenyewe hatupo makini na kile tunachokifanya ndio maan ahatupigi hatua, nchi kama Kenya au Niger wasanii wanafaidika na kazi zao kwasababu wapo makini na wanajua wanachokifanya,” alisema Steve Nyerere.

Alisema anawashukuru Watanzania kwa kumpokea vizuri katika sanaa, ikiwa ni pamoja na kuzipokea vizuri kazi zake na kuwataka wapenzi wa burudani kukaa mkao wa kula kwaajili ya kuzipokea kazi zake nyingine.

“Mwaka huu nimejipanga kutoa kazi nzuri ambazo naamini zitafanya vizuri katika soko hilo ikiwa ni ndani na nje ya nchi, naomba watanzania tushirikiane kuendeleza sanaa ya nchi yetu,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages