January 16, 2013

WAFANYABIASHARA BUGURUNI WATISHIA KULIPA USHURU


N Mwandishi Wetu

WAFANYABIASHARA wa soko la Buguruni lililoko wilayani Ilala jijini Dar es Salaam wametishia kusitisha kulipa ushuru hadi hapo soko hilo litakapoboreshwa miundombinu yake.

Akizunguza na mtandao huu, kwa niaba ya wenzake jijini jana, mmoja wa wafanyabiashara hao, Maulu Mali alisema hawaamini kuwa serikali kuwa haina fedha ya kujenga soko hilo.

Alisema wamefikia hatua hiyo baada ya viongozi mbambali akiwemo Rais Jakaya Kikwete kushindwa kutekeleza ahadi zao za kujenga soko hilo.

Mali alisema hadi sasa wamechoka kudanganywa hivyo ni vema wakasitisha kulipa ushuru hadi hapo watakapohakikishiwa vingine tena kwa vitendo wala si kwa maneno.

Alisema hali ni mbaya katika soko hilo haswa katika kipindi hiki cha mvua, bidhaa za wafanyabiashara hao zinaharibika kutokana na kuvujiwa.

Alisema ndani ya soko hilo hivi sasa kumejaa maji baada ya mifereji ya maji kuziba hali inayohatarisha afya zao.

Alipoulizwa Ofisa Biashara wa wilaya hiyo, Athuman Mbelwa, kuhusu tatizo linalowakabili wafanyabiashara hao, alikirikuwa soko hilo likoa katika hali mbaya likifanana na kiota cha ndege.

Alisema serikali iko mbioni katika kulijenga upya  soko hilo tena kwa kiwango cha ghorofa nne, ambapo anaamini hadi kufikia mwaka 2015 litakuwa limekwisha jengwa.

“Wanajenga jingo hilo ambalo naamini litaweza kuchukua wafanyabiashara wengi na kupunguza usumbufu kwa wafanyabiashara katika wilaya hii”alisema Mbelwa.

Akizungumzia wafanyabiashara wasiyorasmi alisema wanaandaa makubaliano ya pamoja yatakayosaidia pande zote mbili katika kufanya shuhuli zao bila ya athari kati yao.


No comments:

Post a Comment

Pages