January 20, 2013

NSSF YAANZA KUUZA NYUMBA ZA KIBADA


Baadhi ya nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya jikoni
Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula akiangali akikagua nyumba ya shirika hilo kabla ya kuikabidhi kwa mnunuzi wa nyumba hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
Mmeona mandhari ya nyumba ilivyokuwa nzuri
Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula (kulia) akimkabidhi funguo ya nyumba, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid. (Na Mpiga Picha Wetu)
Wakipewa kadi ya Luku
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid akiweka saini baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid. Kulia ni Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula.  
Karibuni ndani

No comments:

Post a Comment

Pages