January 23, 2013

SIJUTII KWA NILIEKUWA NAE


Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Barnaba Elias ‘Barnaba’ ameachia video ya kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Sijutii kwa niliekuwa nae’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Barnaba alisema wimbo huo kaupeleka sokoni wiki iliyopita na kwamba umeshaanza kufanya vizuri katika soko hilo, kitu ambacho kinampa moyo wa kufanya kazi hiyo bila kuchoka.

“Kama kawaida yangu nyimbo zangu nyingi huwa haziwachukizi mashabiki wangu ni jambo ambalo namshukuru mungu kwani ni wasanii wachache ambao nyimbo zao zinafanya vizuri mtaani,” alisema.

Barnaba alisema anawaomba mashabiki wa muziki huo kuendelea kumpa sapoti katika kazi zake ikiwa ni pamoja na kukaa mkao wa kula kwaajili ya kupokea kazi nyingine ambazo zinakuja.

Mbali na kibao hicho, Barnaba alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Magubegube, Wrong number, Tulizana, Milele daima, Sorry na vinginevyo ambavyo vinafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages