January 29, 2013

TANZANIA KUWA CHUNGU CHA KUTOA WATAALAMU WA KUSIMAMIA NGUMI AFRIKA NA ASIA


DAR ES SALAA, Tanzania
TANZANIA inaelekea kuwa chungu cha kutoa wataalamu wa kusimamia ngumi katika bara la Afrika baada ya Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Afrika  kuorodhesha maofisa wa ulingo watakaopata nafasi za kusimamia mapambano kadhaa ya ubingwa katika bara la Afrika.

Katika orodha iliyotolewa na IBF Africa wako watanzania sita ambao IBF imewataja kuwa watakuwa wanapata nafasi za kusimamia mapambano ndani na nje ya bara la Afrika.

Mwaka huu 2013, IBF Africa na IBF Asia zitaanza mapambano ya kuwakutanisha mabingwa wa mabara yote mawili hivyo maofisa watakaosimamia mapambano haya katika bara la Afrika na bara la Asia watatoka katika mabara haya mawili.

Orodha kamili ya maofisa hao inaongozwa na Rais wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi..
(Afrika ya Kusini)  Alfred Buqwana, Wally Snowball, Simon Xamlashe na Jaap Van Niewenhuizen
(Ghana) Rodger Barnor, Fred Ghartey, Confidence Hiagbe na May Mensah Akakpo
(Uganda) Simon Katogole na Ismail Sekisambu.
(Zambia) William Sekeleke and John Shipanuka
(Tanzania) Onesmo Ngowi, Nemes Kavishe, Boniface Wambura, John Chagu, Mark Hatia na mwamuzi anayechipukia kutoka jiji la Tanga Gallous Ligongo,

Kufuatana na orodha iliyotolewa na IBF Afrika, Tanzania inaonekana kuwa na uwezekano wa kutoa maofisa wengi wa ulingo kuliko nchi nyingine za Kiafrika hivyo kuipa nafasi nzuri ya kujitangaza.
Imetolewa na:

UTAWALA
Internatiknal Boxing federation Africa

No comments:

Post a Comment

Pages