January 25, 2013

VIJANA MSIGEUZWE KUWA KALAI LA ZEGE


Na Bryceson Mathias

BIBLIA Katika Timotheo wa kwanza 4:12  inasemaMtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika Upendo na Imani na Usafi.

Ni wajibu wangu sasa kuwaambia vijana nchini msikubali kugeuzwa kuwa kalai la zege, ambalo nyumba ikishakujengwa ikamalizika, linatupwa kuwa ni uchafua linatupwa kuwa  halina maana kwa maana kwamba ni uchafu.

Nasema hivyo kwa sababu, takribani mwaka mmoja hivi, nilisikia kuna watu wanaendeleza na kufadhili mpango (program) ya kufundisha umafia vijana, ambapo inadaiwa walidiriki kuwaweka kambini na na kusemekana kuwalipa shs 30,000/- kwa wiki.

Bahati mbaya nilipofika eneo lililodaiwa kuwekwa vijana hao Katika Kijiji cha Lungo Kata ya Mtibwa wilayani Mvomero, sikuwakuta! Lakini mbali na kutowakuta, nilitaka niwaambie madhara ya kufanywa Kalai la Zege ambalo nyumba ikishakujengwa na kumalizika, linatupwa kuwa ni uchafu.

Vijana; Njaa ya tumbo isiwadhalilishe, wanaowatumia ndio waliowanyima elimu, ndio waliowanyima ajira,ndio waliowanyima mafao mbalimbali wazazi wenu, ndio wanaowanyanyasa walimu na madaktari hata mkakosa huduma muhimu na hatimae tunakufa mapema. 

Vijana mnatakiwa  kuamka (amkeni sasa), maana mnatumiwa vibaya kwa muda tu na baada ya hapo ninyi mnageuka kalai la zege ambalo nyumba ikishakujengwa linatupwa kuwa ni uchafu.

Hakuna mtu asiyejua kuwa vijana mna nguvu. Niseme hivi, ni rahisi zaidi popo kuwa ndege, kuliko ndizi kuwa tunda. Kama mmeelewa hapo, basi vijana msithubutu kukubali kutumiwa na mafisadi kwa ajili ya utawala wa kifisadi ambao unaweza madarakani na mafisadi.

Katika kitabu cha 1yohana 2:14 “Biblia inasema…. Nimewaandikia ninyi,vijana kwa sababu mna nguvu, na Neno la Mungu linakaa ndani yenu ,nanyi mmeshinda yule mwovu (Shetani), na si kufundisha umafia.

Nguvu zinazozungumziwa hapa ni uweza wa Mungu wa kukusaidia kutekeleza maagizo yake. Na kwa sababu hiyo basi kuna matarajio ya Mungu kwa hao vijana na lengo likiwa kwa muda wako mfupi wa maisha ni ni kukueleza nini Mungu anatarajia, anategemea kwako kwamba utafanya sawasawa na nafasi aliyokupa mbele zake.

Matarajio ya Mungu kwa vijana ni kama ifuatavyo: Moja, Vijana wauteke ufalme wake, popote pale vijana walipo, Darasani, Chuoni, Kazini, na Kanisani, hii ni kwa sababu wana nguvu. .

Mbili, Nguvu za Vijana zirejeshe urithi na mali za wana wa Mungu zilizotekwa. Mwanzo 14:13-16. “… . Hizi ni habari za Ibrahamu aliyekwenda kumuokoa nduguye Lutu baada ya kuwa ametekwa.Ili kurejesha urithi wao na mali zao ilimbidi Ibrahimu atumie nguvu kazi ya vijana.
Na hivyo hata leo Mungu anatarajia kwamba vijana wasimame kwenye nafasi zao na kupambana kwa ajili ya afya,ulinzi, uchumi,uponyaji,mafanikio ya watu wake. 

Hebu jipe dakika moja halafu tazama jinsi shetani anavyotesa watu na kudhulumu afya zao, ujana wao, ndoa zao ,uchumi wao, Je, ni nani watakaorejesha hali nzuri, urithi huu kwa wana wa Mungu kama si Mungu kupitia Vijana?. Hivyo vijana hampaswi kutumika kutumika kujifunza kufanya umafia
TatuVijana wasikosee katika kufanya maamuzi ya kuoa au kuolewa. Mithali 5:18 “Chemichemi yako ibarikiwe;nawe umfurahie mke wa ujana wako”.Sikiliza Mungu anataka ndoa yako iwe ya mafanikio na ya furaha, maana yake ndoa ambayo hautaijutia  kwa nini nilimuoa au kuolewa na huyu mtu.

Ili ndoa yako iwe ya furaha na amani, ni lazima huyo mwenzi wako umpate kwa uongozi wa Mungu mwenyewe. Sasa mtazamo wa Mungu kwa vijana ni huu, vijana hawatakosea kufanya maamuzi, wakaamua kujifunza Unafia, maana bado wana wajbu wa kulikomboa Taifa na kurudisha rasilimali kama Twiga, fedha za Uswizi kama Fuvu la Mkwawa lilivvyorudishwa..

Nnevijana wawe wasuluhishi wa matatizo katika jamii na taifa. Mithali 1:4 “Kuwapa wajinga werevu,na kijana maarifa na hadhari”. Leo ndani ya kanisa, Taifa na Jamii tunayoishi,  kwa ujumla yapo matatizo mbalimbali.

Sasa Mungu anatarajia vijana ndio watumike kusuluhisha matatizo haya mbalimbali katika jamii kwa sababu ya wingi wa neno la Kristo ndani yao. Hii ina maana mtu mwenye neno la Kristo kwa wingi ndani yake basi maana yake ana upeo mkubwa wa kuelewa mipango na njia za Mungu za kuwatoa watu wake kwenye matatizo yanayowakabili, ili kuwatoa wake kwenye  shida walizonazo, na si kufanya unafia.

Tano, Vijana walitumikie Taifana Jamii kwa uadilifu na si kwa rushwa na ufisadi. Ni matarajio yake kwamba vijana watapita nyumba kwa nyumba, mtaa hadi mtaa wawaambie wtanzania wawaambie watanzania na wageni juu ya gharama ya Aman tuliyonayo. Naamini haya matarajio matano ya Mungu kwako kwa vijana wenzangu basi yatakusaidi kukaa kwenye nafasi yako ili Mungu ajivunie kuwa na kijana kma wewe badala ya kujiunga na mafisadi.

No comments:

Post a Comment

Pages