Na Elizabeth John
MUIGIZAJI wa filamu za kibongo na mchekashaji,
Tumain Martin ‘Matumaini’ anatarajia kurudi hospitali ya Amana jiijini Dar es
Salaam mara baada ya kumaliza dozi ya dawa alizopewa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, rafiki wa
karibu wa msanii huyo, Robart Kiwewe ‘Kiwewe’ alisema kuwa Matumaini alikaa
hospitalini hapo kwa muda wa siku tatu akiwa anasumbuliwa na miguu ambapo jana
aliruhusiwa kurudi nyumbani.
“Hivi nimetoka nyumbani kwao Yombo kumuangalia
bado hali yake nsio nzuri, daktari kampa dawa kamwambia arudi hospitali baada
ya kumaliza kumeza dawa hizo, Watanzania tunatakiwa kumuombea mwenzetu ili
arudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Kiwewe.
Alisema hali yake sio nzuri kwani hadi sasa
hajui ni ugonjwa gani unaomsumbua, taarifa walizozipata mwanzo ni kwamba
alianza kusumbiliwa miguu ikafuata na mikono na sasa maumivu yamesambaa sehemu
mbalimbali za mwili wake, kutokana na kushindwa kugundua ugonjwa unaomsumbua
daktari ameamua kumpa dawa za kupunguza maumivu.
Kiwewe alisema kwasasa hawana utaratibu mwingine
ambao wameweza kuufanya mpaka amalize kumeza dawa hizo na kurejea tena
hospitali.
Matumaini alikwenda kuishi nchini Msumbiji na
kulipotiwa kusumbuliwa na maradhi lakini alishindwa kutibiwa akiwa huko ambapo
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla alichukua
jukumu la kumpatia nauli ya kumrudisha nchini.
No comments:
Post a Comment