March 26, 2013

BRAZIL, RUSSIA HAKUNA MBABE STAMFORD BRIDGE, ZATOKA SARE YA 1-1

Yoso Mbrazil anayechezea klabu ya Chelsea ya England, Oscar (kulia), akichuana na nyota wa timu ya taifa ya Russia wakati wa mechi ya kirafiki kwenye dimbala Stamford Bridge, jijini London, iliyoisha kwa sare ya bao 1-1
 Mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil, wakifuatilia mtanange huo Drajani jana usiku.
 Mcheza shoo akitumbuiza mashabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Stamford Bridge kufuatilia mechi kati ya Brazil na Russia.
Beki wa timu ya taifa ya Brazil, David Luiz (kulia), akizuia shuti la kiungo Yury Zhirkov wa timu ya taifa ya Russia, wakati wa mechi ya kirafiki kati ya nchi hizo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London, Uingereza na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
 Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil, wakishangilia bao la timu yao ilipoumana na Russia jana usiku.
 Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil, wakishangilia bao la timu yao ilipoumana na Russia jana usiku.
Victor Fayzulin wa Russia (20) akifunga bao kunako dakika ya 73 ya pambano la kirafiki dhidi ya Brazil kwenye dimba la Stamford Bridge jijini London jana usiku.
Victor Fayzulin wa Russia (20) akifunga bao kunako dakika ya 73 ya pambano la kirafiki dhidi ya Brazil kwenye dimba la Stamford Bridge jijini London jana usiku.
 Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil, wakishangilia bao la kusawazisha lililofungwa na Fred (katikati).
 Mshambuliaji wa Brazil, Fred (9), akifunga bao la timu yake katika mechi hiyo ya kukata na shoka.
 Fred (9), akishangilia bao lake huku akimfuata David Luiz.
Polisi akimfukuza ili kumkamata shabiki huyu wa soka ambaye hakujulikana jina, baada ya kuingia uwanjani wakati huo Russia ilikuwa mbele kwa bao 1-0. Dakika chache baada ya shabiki huyu wa Russia kuingia, kisha kutolewa uwanjani, Brazil ikasawazisha bao.

No comments:

Post a Comment

Pages